Tuesday, November 6, 2012

JAMAA AMFUMANIA MKE WAKE AKIFANYA MAPENZI NA BABA MWENYE NYUMBA..

Niaibu iliyoje huku.......
                                    Tukio hili limetokea usiku wa kuamkia leo,maeneo ya manzese tip top karibu na shule ya msingi MPAKANI ..mara baada ya ndugu MAULID  KASIM  mkazi wa maeneo hayo kupewa taarifa na watu ambao alishindwa kuwataja kwa majina kumpigia sim na kumueleza kuwa mke wake amejitanua kwenye kitanda cha 6kwa6 na baba mwenye nyumba yake..BOY NASRI  ilipo jikita katikati ya tukio hili akamtafuta ndugu MAULID nakuzungumza nae .......
kaka inakuaje hapa mbona jazba sana ..tulimuuliza hivi na jamaa akaanza kutiririka kwa jazba......!

"nisiku nyingi sana nilikuwa nikisikia hizi tetesi lakini sikutaka kukurupuka pia marakwa mara nikimuuliza mke wangu huwa anakataa katakata..sasa leo wakati nipo job jamaa yangu mmoja ambae tunaishi maenei jirani na hapa kwetu..alinipigia sim nakuniambia kuwa nyumba yako imeingia nungunungu mda simrefu...daaah...kiukweli niliishiwa na nguvu zote ilibidi nichukue piki piki hadi hom ,nilipofika pale ndani sikutaka kuuliza zaidi ya kuchukuwa jiwe na kuvunja mlango..sikuamini kabisa macho yangu kwa mambo niliyo yakuta na kuyaona humo ndani.hasira zilinipanda nikajikuta namtia makonde na vitasa vya uso huyo mzee..kiukweli kama sio hawa wapangaji kuja kugombelezea huyu mzee nilitaka kumuua...kwani nilisha chukuwa panga na rungu ambalo nililificha nyuma ya mlango..."

Duuuuh..huyo mzee ni mara ya kwanza kutembea na mke wako au ndio tabia yake...?

Huyu mzee ni mshenzi sana ,hata mimi nilisha pata story yakuwa ndio kawaida yake kutembea na wake za watu. ila mimi lazima nitamkomesha tu kama ndo anaringia hilo banda la kufugia kuku mimi sibabaishwi na gofu kama hili ..kwasababu kwetu kunamjengo zaidi ya kibanda hiki...

wakati vurugu zikiendelea boy nasri ilifanya jitihada za kumtafuta huyo mzee ili kufanya maojiano nayo..kwa bahati mbaya haikuweza kumkaribia ila ilimshuhudia kwa mbali akimiminika dama huku amevimba karibu sehemu zote za mwili....ilipofika majira ya saa5 usiku polisi waliwasili maeneo hayo na kuwa chukuwa wote kwenda kufanya mahojiano nao...

baadhi ya watu waliokuwa maeneo hayo wakishuhudia tukio hilo walisema kuwa mke wa huyo jamaa ndie anastahili kupewa lawama zote ..ingawaje baadhi yao wakimtupia lawama huyo mzee....


1 comment: