MADAKTARI wametangaza kuanza kwa mgomo kesho mpaka hapo serikali itakapokuwa tayari kutekeleza madai yao.
Pia
wamesema kuwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, amelidanganya Bunge kwa kusema
kuwa madai ya madaktari tayari yameshashughulikiwa wakati siyo kweli.
Hayo
yalisemwa jana na kiongozi wa Jumuiya ya Madaktari nchini, Dkt. Steven
Ulimboka, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es
Salaam
Amesema kuwa, hadi sasa hakuna makubaliano yoyote
yaliyofanyika kuhusiana na madai ya madaktari yaliyokuwa
yakilalalamikiwa nyuma.
Amesema Awali madaktari hao walikubali
kurudi kazini kwa kuwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, aliwataka kurejea
kazini kwa ahadi ya kushughulikia madai yao
Amesema hayo
yamekuja baada ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kulidanganya Bunge kwa
kusema kuwa madai ya madaktari tayari yameshashughulikiwa wakati siyo
kweli.
“Waziri Mkuu, amelidanganya Bunge wakati akijibu maswali
ya papo kwa hapo, kwa kusema kuwa madai kumi waliyowasilisha, matano
yameafikiwa na kila upande” jambo ambalo si kweli.
Pinda alilieleza Bunge kuwa serikali iliunda kamati maalumu ya kushughulikia madai yao kumi, matano yameafikiwa na kila upande.
“Baada
ya hatua zote hizo kwa mujibu wa sheria ni lazima makubaliano yao
yasajiliwe na Tume ya Usuluhishi (CMA), na kwamba hilo limefanyika
ambapo tume ya serikali na upande wa madaktari wamemaliza kazi yake.
“Kati
ya madai waliyoyataka serikali imeyatekeleza ni pamoja na kuondolewa
kwa mawaziri wa wizara hiyo, kuongezwa posho ya kuitwa kazini, kufanya
uchunguzi wa maiti na nyinginezo,
“Mambo matano waliyoafikiana ni
serikali kukubali kuongeza posho ya kuitwa kazini kutoka sh 10,000 hadi
sh 15,000 kwa madaktari walio kwenye mafunzo kazini na sh 20,000 kwa
madaktari na sh 25,000 kwa madaktari bingwa.
“Pia serikali
iliongeza posho ya uchunguzi wa maiti kutoka sh 10,000 hadi 100,000 kwa
madaktari na sh 50,000 kwa wasaidizi, alisema Waziri Mkuu Pinda.
Ikiwemo
na serikali kukubali kuwapa kadi ya Bima ya Afya ya rangi ya kijani
ambayo ina hadhi ya huduma za daraja la kwanza kwa madaktari, pia kutoa
chanjo ya ugonjwa wa ini ambapo fedha za chanjo hiyo zimo kwenye bajeti
ya mwaka ujao wa fedha 2012/2013.
Hata hivyo, maelezo hayo yalipingwa vikali na Chama cha Madaktari (MAT) na kupeleka kutangaza mgomo huo jana
Akiongea
wakati akitangaza mgomo huo kwa niaba ya madaktari wenzake, Ulimboka
alisema kuwa katika madai yote ya madaktari hakuna dai hata moja ambalo
limetekelezwa kama alivyoeleza Waziri huyo
No comments:
Post a Comment