Monday, August 27, 2012

Tamaa ya Makalio Makubwa Yamtokea Puani, Akatwa Mikono na Miguu



NewsImages/6445306.jpg
April Brown amepoteza mikono na makalio yake kutokana na sindano za kuongeza makalio
Thursday, May 31, 2012 12:11 PM
Mwanamke mmoja wa nchini Marekani ambaye alikuwa na ndoto ya kuwa na makalio makubwa amejikuta akikatwa miguu yake yote miwili na mikono yake yote miwili baada ya kupata maambukizi wakati alipopigwa sindano ya kuongeza ukubwa wa makalio.
April Brown mkazi wa jiji la Los Angeles nchini Marekani ambaye pia ni mama wa watoto wawili, alinusurika kufariki dunia baada ya kudungwa sindano ya kuongeza makalio ili awe na makalio makubwa kama ya mastaa wa Marekani kama vile Jennifer Lopez, Nicki Minaj na wengine.

Tamaa yake hiyo ya kuwa na makalio makubwa ilimponza na kupelekea apoteze mikono yake yote miwili na miguu yake yote miwili baada ya kupata maambukizi ambayo yalitishia uhai wake na kupelekea madaktari walazimike kuvikata viungo vyake.

Bi Brown amesema kuwa alidungwa sindano hiyo ya kuongeza ukubwa wa makalio yake na baada ya sindano hiyo alibaki na maumivu makali sana yaliyomsumbua kwa muda mrefu.

Bi Brown ambaye awali alikuwa ni mwanamitindo alisema kuwa sindano aliyodungwa kwenye zahanati bubu za kuongeza makalio ilitakiwa kuwa na silikoni maalumu inayotumika kwaajili ya matibabu lakini badala yake alidungwa sindano ambayo ilikuwa na kiasi kikubwa cha silikoni inayotumika viwandani.

Bi Brown amegoma kuitaja zahanati hiyo feki aliyoenda akisema kuwa wa kujilaumu ni yeye mwenyewe kwa tamaa yake ya kuongeza ukubwa wa makalio yake.

Hivi sasa bi Brown anaendesha kampeni ya kuwaonya wanawake juu ya madhara ya njia hiyo ya kuongeza ukubwa wa makalio.

Angalia VIDEO ya bi Brown alivyo sasa na jinsi anavyojaribu kuyaendesha maisha yake katika hali yake hii mpya.

No comments:

Post a Comment