Saturday, September 22, 2012

Ajifungua akiwa kwenye chumba cha mtihani wa kumaliza darasa la 7


MWANAFUNZI wa kike wa Shule ya msingi Kabiri iliyopo Kata ya Kabirizi Wilayani Muleba Mkoani Kagera amejifungua akiwa katika chumba cha kufanyia mtihani wa kuhitimu elimu ya msing
 Msichana huyo [14] jina limehifadhiwa, ambaye alikuwa akifanya mtihani wake wa darasa la saba, alianzwa na hali ya uchungu akiwa katika chumba cha mtihani na hatimaye kujifungua mtoto

Awali ilidaiwa kuwa, mwanafunzi huyo alimuomba msimamizi wake aende msalani akajisaidie na msimamizi huyo alimruhusu, hivyo kudaiwa baada ya dakika chache alimuomba tena msimamizi huyo ruhusu aende nje lakini ilidaiwa msimamizi hakumruhusu kwa kudhani huenda mwanafunzi huyo alikuwa anafanya ujanja wa kupata majibu ya mitihani

Imedaiwa msimamizi huyo alimzuia mwanafunzi huyo asitoke lakini baadae msimamizi huyo alianza kuingiwa na wasiwasi kwa kuona binti huyo anajinyonga zaidi na kumuuliza anasumbuliwa na nini na mwanafunzi kudaiwa alimjibu anasumbuliwa na tumbo

Lakini jibu hilo halikumtosheleza msimamizi huyo kwa kuona msichana huyo anazidi kujinyonga nyonga, aliendelea kumuuliza linamuuma vipi ndipo mwanafunzi huyo alimwambia ukweli msimamizi huyo kwa kumwambia anaumwa na uchungu

Msimamizi huyo ndipo alipoanza kufanya juhudi za kutafuta msaidizi ili wamsaidie binti huyo lakini baadae binti huyo alifanikiwa kujifungua mtoto wa kiume akiwa katika chumba hicho

Taarifa hizi zimethibitishwa na uongozi wa shule ikiwemo Afisa Elimu wilayani humo akiwemo Mkurugenzi Halmashauri ya Kagera

No comments:

Post a Comment