China: Mama wa mapacha wanne aamua kuwanyoa wanae kwa staili ya namba ili kuwawezesha walimu kuwatambua..VIDEO
Tan Chaoyun ni mama wa mapacha wanne ambao wamefanana sana kiasi cha
kumchanganya hata yeye mwenyewe. Imefikia wakati mmoja wao anaweza fanya
kosa lakini akajikuta anamuadhibu mwingine kwa jinsi walivyo fanana.
Mama huyo aliongeza kuwa ni afadhali yake ila baba yao ndiyo hawezi
kabisa kuwatofautisha. Hata shuleni walimu wamekuwa wakipata tabu sana kuwatofautisha.
Ila kuwasaidia walimu katika hilo, mama huyo aliamua kuwanyoa watoto
wake kwa staili ya namba 1 hadi 4 ili kuwarahisishia walimu kuwatambua
watoto hao.
No comments:
Post a Comment