Sunday, September 16, 2012

Kagera: Binti achunwa ngozi na mwili kutelekezwa porini

Tukio hili la kusikitisha limetokea kijijini Mayondwe Muhutwe jimbo la Muleba Kaskazini mkoani Kagera,pale mwili mtoto Beatha (12) ulipokutwa umetelekezwa porini huku ukiwa umechunwa ngozi na kuondolewa sehemu zake za siri.
Polisi inamshikilia mzee mmoja anaye husishwa na matukio ya uchunaji ngozi za binadamu. Pamoja pia imeelezwa kuwa kuna baadhi ya watu wanaoshukiwa kuhusika na tukio hilo lakini wanaachiwa kirahisi na polisi wa eneo hilo.
Kushoto ni daktari aliyethibitisha tukio hilo akisaidiana na polisi kubeba mwili huo ili kuuhifadhi kwenye sanduku.

No comments:

Post a Comment