Askari
wa Kikosi cha Polisi cha Kutuliza Ghasia (FFU), wakiwa kwenye gari
wakifanya doria Dar es Salaam leo, baada ya kuwepo njama ya baadhi ya
Waislam kuandamana kutaka kumg'oa madarakani Mufti wa Tanzania, Sheikh
Issa Bin Shaaban Simba. (picha: Habari Mseto Blog)
Baadhi ya waislamu wakiwa nje ya msikiti wa Mtambani, Kinondoni, Dar es Salaam baada ya kuswali leo (picha: Habari Mseto Blog)
Na Andrew ChaleJESHI la Polisi nchini limefanikiwa kudhibiti maandamano yaliyokuwa yamepangwa kufanyika jijini Dar es Salaam, ya kushinikiza kumuondoa Mufti wa Tanzania, Sheikh Mkuu, Issa bin Shaaban Simba, Katibu Mkuu wa Baraza la Taifa la Mitihani (NECTA), Dkt. Joyce Ndalichako na Ubalozi wa Marekani.
Jeshi hilo lilifanikiwa kuzima maandamano hayo, licha ya waislamu kukaidi agizo hilo la kuwataka wasifanye hivyo na hiyo juzi na Kamanda wa Polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova.
Waislam hao ambao walipanga maandamano hayo hiyo jana baada ya ibada ya Ijumaa, na kuwatangazia waumini wao kujitokeza kwa wingi licha ya kupigwa marufuku, na kusambaza vipeperushi mitaani kuwataka kufanya hivyo.
Tanzania Daima, liliweza kushuhudia magari ya jeshi la Polisi zaidi ya 8, yakiwemo ya maji ya machozi,kikosi cha kutuliza ghasia na FFU, Polisi wa kawaida na kikosi cha mbwa wakizunguka mitaa mbalimbali ya katikati ya jiji majira ya saa nne, asubuhi yakizunguka na kisha kuelekea a barabara ya Morogoro na kutokomea kusiko julikana.
Hata hivyo, gazeti hili, lilishuhudia Polisi na makachelo waliovalia mavazi ya kawaida wakiwa wamemwaga kila kona kuimalisha usalama ikiwemo makao makuu ya Bakwata, ambapo pia kuna msikiti mkubwa waumini mbalimbali walikuwa wakiendelea kusali sala ya Ijumaa.
Kwa upande wake, Shehe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhadi Musa Salum aliwataka waislamu kuungana kwa pamoja na kulaani watu wanaokashifu uislamu kwa maslai yao binafsi ikiwemo suala la Raia wa Marekani kumkashifu Mtume kwa kupitia filamu aliyoitengeneza hivi karibuni.
“Naungana na waislamu wote kulaani kitendo hichi kwani kinaweza kuleta uvunjikaji wa amani duniani” alisema Alhadi Musa.
Pia alisema kuwa, waislamu wanapaswa kukemea jambo hili kwa nguvu zote kwa mlengo wa amani pasipokuleta machafuko.
Aidha, Kwa upande wa msikiti wa Mtambani, Masjid Mtambani, jeshi la Polisi liliweza kujipanga kila kona huku magari mawili ya FFU yakiwa yamejipanga kukabiliana na hali yoyote ya hatari.
Gazeti hili lilishuhudia umati mkubwa uliokuwa ndani licha ya kumalizika kwa sala ya Ijumaa, wakiendelea kusikiza mawaida ambayo asilimia kubwa yalikuwa kisisitiza kuondolewa kwa Mufti Simba na watu wake sambamba na kupinga NECTA na Ubalozi wa Marekani. Hata hivyo vyanzo mbalimbali vya habari ambavyo vilipatikana eneo la tukio, ikiwemo kutoka kwa waumini hao kwenye msikiti wa Mtambani, zilidai kuwa licha ya jesjhi la Polisi kuzuia maandamano yao ya kumuondoa Mufti Simba, yapo pale pale.
“Kuuondoa utawala wa Bakwata upo pale pale, waislamu tushikamane hilo jeshi la Polisi ipo siku nao watajua nini tunafanya” kilisika chanzo cha habari.
Pia uchunguzi wa gazeti hili ulishuhudia kila msikiti kuwa na jeshi waliokuwa nje ya misikiti hatua tano na magari yao wakilinda usalama hali ambayo ilizua hofu kwa kila mpita njia ambayo kwa hali ya kawaida ilionekana kama katika misikiti ya nchi za uarabuni pindi kunapokuwa na machafuko.
Mbali na hilo, pia katika maenei ya Ubalozi wa Marekani gazeti hili lilishuhudia jeshi la Polisi likiwa limeweka doria mbali na wale wanaolinda ubalozi huo mara kwa mara.
Awali onyo la Kova kwa wananchi na wafuasi wa vikundi hivyo vya kiislamu ambavyo si rasmi, wasifuate mkumbo katika kutekeleza azma hiyo ya kuandamana, kwani yeyote atakayeshiriki atakamatwa na kuchukuliwa hatua kali za kisheria mara moja.
Vuguvugu la kuuondoa uongozi wa Bakwata zinadaiwa kuwa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu lililo chini ya Shehe Ponda Issa Ponda na wenzake kushinikiza kuondolewa kwa kushindwa kuwajibika ikiwemo juu ya wanafunzi wa kiislamu kufelishwa mitihani yao na NECTA.
Via: wavuti.com
No comments:
Post a Comment