MWALIMU
wa Shule ya Msingi Magamba, wilayani Handeni, amehukumiwa kutumikia
kifungo cha miaka mitatu jela, baada ya kupatikana na hatia ya kufanya
mapenzi na kumpa mimba mwanafunzi.
Mwalimu
huyo, Daniel Lukindo (24), alikuwa anakabiliwa na mashtaka ya kumpa
mimba mwanafunzi Halima Rashidi wa kidato cha nne katika Shule ya
Sekondari ya Kwaluguru.
Akisoma mashtaka katika shauri hilo
namba 240 la mwaka huu, Mwendesha Mashtaka, Mkaguzi Msaidizi wa Polisi
Elibaliki Polanjo, alieleza mahakama kuwa kati ya Novemba mwaka jana na
Februari mwaka huu katika Kijiji cha Magamba, mwalimu Lukindo alikuwa
akifanya mapenzi na mwanafunzi huyo na baadaye, kumpa ujauzito.
Katika kesi hiyo iliyokuwa chini ya
Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Handeni, Patrick
Maligana, mshtakiwa alikiri kosa lake, akikubaliana na maelezo yote
yaliotolewa na mwendesha mashtaka.
Kufuatia hatua hiyo, Hakimu Maligana, alimtia hatiani na kumhukumu kutumikia adhabu ya kutumikia kifungo cha miaka mitatu jela.
Akifafanua kuhusu adhabu hiyo,
Maligana alisema mshtakiwa alitenda kosa baya na hasa ikizingatiwa
kwamba ni mwalimu anayepaswa kuwa mfano mzuri katika jamii, kwa kuzuia
na kukomesha wimbi la matukio ya wanafunzi wa kike kupata mimba.“Sheria
inasema mwanaume yeyote atakayempa mimba mwanafunzi atakuwa ametenda
kosa na kama atapatikana na hatia, atastahili kutumikia kifungo
kisichopungua miaka mitatu jela na kisichozidi miaka sita. Kosa hili
halitakuwa na nafasi ya kulipa faini,” alisema Maligana.
Alisisitiza kwamba adhabu hiyo alitoa
itakuwa fundisho kwa walimu na wanaume wengine wenye tabia ya kupenda
kufanya mapenzi na wanafunzi wa kike.
No comments:
Post a Comment