Sunday, September 16, 2012

WANAFUNZI NA PICHA ZA UCHI


Wakati mwingine nikifikiria huwa naumia sana.Siku zote najiuliza ni kitu gani kimetufikisha hapa tulipo? Ni tamaa, ulimbukeni au ndo umaskini unatutesa?.
Najaribu kuangalia mbali lakini sioni tumaini lolote. Naona tumetandwa na giza nene na hatujui nini cha kufanya.....
Kama utakumbuka, tumewahi kuripoti juu ya sakata la POLISI WA KIKE KUPIGA PICHA AKIWA UCHI.
Hatukuishia hapo, tuli ripoti tena juu ya sakata la KIGOGO WA SERIKALI (MKE WA MTU ) KUFUMWA GESTI NA MUME WA MTU........
Nakumbuka pia tumewahi kuripoti juu ya sakata la MZEE MMOJA ALIYEFUMWA GESTI NA MWANAFUNZI....
Bado tuliendelea kuripoti juu ya sakata la WANAFUNZI WA CHUO KIKUU WALIOJIREKODI WAKIFANYA UCHAFU NA WENGINE AMBAO WALIAMUA KUJIUZA......
Kama haitoshi, bado tuliendelea kuripoti juu ya UCHAFU MBALI MBALI WA WASANII WA HAPA NCHINI ambao wamekuwa wakipiga picha chafu na kuziachia mitandaoni..
Leo hii hadi wanafunzi wa sekondari nao wameiga???.....Nani alaumiwe? Askari ambaye pengine anajukumu la kulinda sheria naye anapiga picha chafu.
Mzazi ambaye ni mlezi anaamua kutembea na mwanafunzi,tena wa kidato cha pili........
Ndugu zangu, japo ni mambo ya kawaida kwa wengine, lakini ukweli ni kwamba hali inatisha sasa. Hali ni mbaya jamani.
Huyu ni mwanafunzi ambaye ni nguvu kazi ya taifa. Hili ni taifa gani tunaloliandaa?.....
Unamaoni gani msomaji wetu ambayo pengine yatasaidia kurejesha heshima yetu?
MSIMAMO WETU:
 Tutaendelea kuwaumbua wote wapiga utupu bila kujali umaarufu,pesa walizo nazo au ngazi zao za uongozi

No comments:

Post a Comment