Tuesday, October 16, 2012

Hivi huyu Diamond yupo sawa kweli...?


Mimi ni mmoja kati ya wadau ambao husifia sana kazi za Diamond. Ni kweli amekua akifanya vizuri kwenye Audios, Videos, hata live performance. Ila kwa hili tukio alilolifanya kwenye Fiesta 2012 ndani ya Leaders Club nimeshindwa kuelewa alikua na nia gani. Huwa sipendi kumlaumu mtu moja kwa moja sababu huwezi fahamu nini hasa kilimpelekea kufanya hiviyo. Ila kwa haraka  haraka naweza sema hakutumia busara kufanya hivyo jukwaani.
Maswali nijiulizayo:-
  1. Alikua anatangaza biashara ya mavazi hayo baada ya kuahidiwa pesa nyingi?
  2. Aliamua kufanya hivyo kupagawisha mashabiki?
  3. Bombe au kilevi chochote kingine ndicho kilimpelekea kufanya hivyo?

No comments:

Post a Comment