’Huyo rafiki yake na baba, akamwabia baba yangu kwamba, ana kijana wake anataka kuoa. Baba akamwambia(rafiki yake), kwamba ampatie mahari kwani nyumbani kwake ana binti na ndiyo mimi. Hilo walikubaliana huko klabuni,’’alisema Sikitiko.
Geita – SERA ya mtoto
ya mwaka 1996 inasema kuwa mtoto ana haki ya kulindwa na kuendelezwa
kielimu ili akue vyema kiakili, kimwili, koroho na kimaadili ili awe
raia mwema anayewajibika kwake mwenyewe na taifa kwa jumla.
Hata hivyo hali hiyo ni tofauti kwa baadhi ya wazazi na walezi
walio na jukumu la kutimiza hayo ambao huwageuza watoto kuwa ni miradi
kwa kuwafanyisha kazi ngumu na biashara ndogo ndogo huku wengine
wakikatisha masomo ya watoto hao na kuwaozesha.
Sikitiko Mateso(16), mkazi wa Mtaa wa Rosuti, Wilaya ya Tarime,
mkoani Mara ni mmoja wa watoto waliotendewa kinyume na sera hiyo ya
mtoto, ambapo baba yake mzazi alimlazimisha kuolewa.
Akiwa ndiyo kwanza amehitimu elimu ya msingi mwaka huu wa 2012 katika Shule ya Msingi Mseto, wilayani Geita, mkoani Geita, Sikitiko alisoma kwa msaada wa Shirika la New Light Children Centre Organisation (NELICO), ndoto yake ikiwa kuwa Mwanasheria.

Akizungumza na mwandishi wa makala haya mjini Geita, Sikitiko
alisema kuwa yeye ni mtoto wa kwanza kati ya watoto tisa wa familia ya
mzee Tamaa Mateso mkazi wa mjini Tarime, familia ambayo hutegemea
vibarua vya kulima ili kupata mahitaji ya chakula, mavazi na mahitaji
mbalimbali ya kifamilia na kwamba lengo kubwa la kuwa mwanasheria ni
kujikita katika kupinga ukatili unaowakumba watoto.
Ndoto hiyo ya Sikitiko inatokana na kunusurika kifo, baada ya
kufanyiwa ukatili wa kukatwa masikio na baba mkwe wake, baada ya kukataa
kuolewa kwa nguvu na kijana wake wakati huo akisoma darasa la tatu
Shule ya Msingi Roseti, wilayani Tarime mkoani Mara.
Anasema kuwa baba yake, mzee Tamaa, aliandaa mazingira ya yeye
kuolewa baada ya rafiki yake kumpa taarifa kwamba alikuwa anatafuta
binti wa kuolewa na kijana wake, mazungumzo aliyodai yalifanyika kwenye
klabu ya pombe za kienyeji.
Akisimulia mkasa huo Sikitiko alisema kuwa akiwa na umri wa miaka
13 ambapo alikuwa darasa la tatu katika shule hiyo ya msingi, baba yake
alikuwa akinywa pombe za kienyeji klabuni na rafiki yake aliyemtaja kwa
jina moja la Kipanga.
‘’Huyo rafiki yake na baba, akamwabia baba yangu kwamba, ana kijana wake anataka kuoa. Baba akamwambia(rafiki yake), kwamba ampatie mahari kwani nyumbani kwake ana binti na ndiyo mimi. Hilo walikubaliana huko klabuni,’’alisema Sikitiko.
Baada ya makubaliano ya wazee hao, Tamaa aliporudi nyumbani alimwambia Sikitiko anayetambulika pia kwa jina la Rozi kwamba aolewe.

‘’Alipofika nyumani aliniita; “Rozi’’, akaniambia; “Mwanangu nataka uolewe.”
Anaongeza kuwa: “Nilikataa ombi la baba, nikamwambia mimi bado mdogo sana, pia ninasoma darasa la tatu hivyo, siwezi kuacha shule na kuolewa. Baba alikasirika sana.’’
Anaongeza kuwa: “Nilikataa ombi la baba, nikamwambia mimi bado mdogo sana, pia ninasoma darasa la tatu hivyo, siwezi kuacha shule na kuolewa. Baba alikasirika sana.’’
Anaeleza kuwa baada ya kukataa ombi la kuolewa, baba yake alimpa
amri akitaka aolewe kwa nguvu, huku akimwambia kwamba, atake asitake,
ataolewa na huyo kijana mkazi wa Nyamihutwa Tarime, aitwaye Luis Kipanga
.
Sikitiko alisema kuwa baba yake alivyozidi kuwa mkali baada ya yeye kukataa ombi lake, Juni 2008 aliamua kutoroka nyumbani kwao na kuanza safari ya kutembea kwa miguu muda wa saa 11 kwenda kwa mjomba wake eneo la Chibumbai, Tarime.

Hata hivyo, anasimulia kuwa wakati akitoroka, baba yake alikuwa
tayari ameshapokea mahari ya Sh300,000 kutoka kwa rafiki yake ili yeye
(Sikitiko) aache shule na kwenda kuolewa na kijana huyo.
Anabainisha kuwa baada ya mzee Tamaa kupokea mahari hiyo, mzee Kipanga alimbana ili amtoe yeye kwa ajili ya ndoa, kwani kijana wake(Luis), alikuwa ameshajiandaa kwa mapokezi na kuoa.
Hata hivyo, jitihada za Sikitiko kujiokoa na janga hilo kwa kutoroka nyumbani kwao na kwenda kuishi mafichoni kwa mjomba wake, hazikuzaa matunda kutokana na baba yake kumsaka kila wanapoishi ndugu zake hadi alipomkuta kwa mjomba wake.

‘’Nilikaa kwa mjomba mwezi mmoja na baba alivyonipata, mbele ya
mjomba alinidanganya kwa kuniambia turudi nyumbani nikaendelee na
masomo, kwani ameirudisha ile mahari iliyotolewa na rafiki yake.’’
“Bila kujua kitakachonipata nilikubali na kuongozana naye hadi nyumbani. Lakini baada ya kufika nyumbani, baba aliniambia kuwa ananipeleka moja kwa moja kwa rafiki yake, ili nikaolewe na kijana wake.”
‘’Tulifika nyumbani kwa rafiki yake baba, ilikuwa saa 2:00 usiku. Baada ya kufika, baba aliniacha hapo nyumbani kwa Luis,’’ anaeleza.

Baada ya kuachwa hapo, siku hiyohiyo mkasa ulianza ambapo mzee
Kipanga alimwambia Sikitiko kwamba hawezi kuacha kuolewa na kijana wake
ambaye alikuwa amejiandaa kuoa baada ya kutoa mahari nyumbani kwao.
“Kama huwezi kuolewa na mwanangu, nakukata masikio yote. Huwezi kukataa kuolewa na Luis, wakati nimetoa mahari nyumbani kwenu. Hilo haliwezekani, lazima uolewe na huyu kijana wangu,’’ alisema Sikitiko akikariri maneno aliyoambiwa na mzee Kipanga.

Anasimulia kwa uchungu kuwa baada ya kauli hiyo Kipanga alimwambia
Luis amfunge kamba Sikitiko mikono na miguu kwa pamoja na kamba hiyo
ilipitishwa kwenye mti wa mpapai, kisha wakamlaza kifudi fudi kabla ya
kutekeleza kauli yake.
Sikitiko anasimulia kuwa ilikuwa ikielekea saa tatu usiku wa
asiyoikumbuka ya mwezi Agosti, mwaka 2008, ambapo akiwa amelala
kifudifudi chini ya mti wa mpapai huku akipiga mayowe kuomba msaada,
Kipanga alimkata masikio yote mawili na kumjeruhi mabega na vidole vya
mkono wa kulia kwa kisu chenye incha kali.
Alizidi kusimulia kuwa, baada ya mwanaume huyo kumfanyia ukatili
huo, alimfungua kamba, kisha akamfukuza nyumbani kwake na kumtaka atoke
akisema kuwa amekipata alichokuwa akitafuta kwa kukataa kuolewa.
‘’Baada ya kunikata masikio aliniambia hayo ndiyo niliyoyataka kwa kutaa kuolewa na kijana wake na kunifukuza akitaka niende kwetu,” alisimulia kwa uchungu Sikitiko akiongeza:
‘’Baada ya kunikata masikio aliniambia hayo ndiyo niliyoyataka kwa kutaa kuolewa na kijana wake na kunifukuza akitaka niende kwetu,” alisimulia kwa uchungu Sikitiko akiongeza:
“Wakati huo, damu nyingi ilikuwa ikivuja masikioni, mabegani na
vidole nilivyojeruhiwa na nilijaribu kukimbia nikaanguka chini na
kupoteza fahamu kutokana na maumivu na kuvuja kwa damu, hadi
nilipojikuta niko katika Hospitali ya Wilaya ya Bomani.
Anasimulia kuwa alikaa katika hospitali hiyo kwa muda wa mwezi
mmoja akipatiwa matibabu chini ya msaada wa Kituo cha Kivulini cha
jijini Mwanza na baadaye alihamishiwa katika Hospitali ya Rufaa ya
Bugando, ambapo alifanyiwa upasuaji.
‘’Nikiwa Bugando, walinifanyia upasuaji wa masikio kwa kutoa kipande cha nyama ya paja kisha wakaibandika masikioni, ikashonwa ili kurejesha hali ya sikio,’’ anaeleza.
Kuhusu kusikia, Sikitiko alisema kuwa anasikia vizuri kama watu wengine wenye masikio na kwamba hana tatizo la kutosikia, kinyume na alivyotarajia awali, huku akitoa shukrani kwa Kituo cha Kivulini na Shirika la NELICO kwa msaada wanaompatia ili kuendelea na masomo yake.

Mkurugenzi wa NELICO, Paulina Alex alisema kuwa walimpokea Sikitiko
mwaka 2009 na kumpeleka katika Shule ya Msingi Mseto kuendelea na
masomo yake darasa la nne na kwamba maendeleo yake kimasomo ni mazuri,
yanayoweza kumsaidia kutimiza ndoto yake kuwa mwanasheria.
‘’Kwa kweli Sikitiko (Rozi) tuko naye tangu tulipompokea, anaishi
vizuri na wenzake na maendeleo yake kimasomo ni mazuri. Sisi NELICO,
tutamsaidia kumsomesha, pia kumpatia elimu ya kisaikolojia, ambayo
imemsaidia kuishi vizuri na wazazi wake wakati anapoenda
likizo,’’alisema Alex.
Kuhusu hatua zilizochukulia dhidi ya mhusika wa tukio la kumkata
masikio kwa binti huyo, Alex alisema kuwa mtuhumiwa wa kitendo hicho
alikamatwa na kufunguliwa kesi ya jinai katika Mahakama ya Wilaya ya
Tarime na kwamba Shirika la Kivulini, ndilo linalohusika kufuatilia
mwenendo mzima wa kesi hiyo.
Sikitiko alisema kuwa anatarajia kufaulu katika mtihani wa Taifa wa Darasa la Saba mwaka huu akisisitiza kwamba ndoto yake ni kusoma hadi chuo kikuu.
Sikitiko alisema kuwa anatarajia kufaulu katika mtihani wa Taifa wa Darasa la Saba mwaka huu akisisitiza kwamba ndoto yake ni kusoma hadi chuo kikuu.
‘’Napenda masomo yote, darasani nilikuwa nashika nafasi ya kumi
mwisho 18 kati ya wanafunzi zaidi ya 100, kwa hiyo ninatarajia kushinda
kwenda sekondari, ndoto yangu ni kwenda chuo kikuu niwe mwanasheria,
ambaye nitasaidia watoto wanaoonewa na kufanyiwa ukatili,’’alisema
Sikitiko.
Majina yaliyotumika katika makala haya ni ya kubuni ili kulinda hadhi ya mtoto
No comments:
Post a Comment