Tukio hili limetokea mji wa Wenling huko China baada ya wamiliki (Bw.Luo Baogen na mkewe) wa jengo kuikatalia serikali kubomoa nyumba yao ili kupisha ujenzi wa barabara. Wamiliki hao walidai kuwa fidia iliyo tolewa na serikali ni ndogo ukilinganisha na thamani ya nyumba, hivyo hawawezi kujenga nyumba nyingine kama hiyo. Wakazi wengine wa jirani walikubali kuhamishwa na kulipwa fidia yao.
Tofauti na ilivyo kuwa miaka ya nyuma, kwa sasa sheria ya ubomoaji makazi ya mtu huko China imemlinda sana mmiliki. Kwani serikali haiwezi kubomoa nyumba ya mtu kwa nguvu bila yeye kuridhia. Hivyo ukionacho pichani ndicho kilichofanyika baada ya kutofikia muafaka.
Hapa Bw.Luo Baogen akiangalia barabara toka kwenye dirisha la nyumba yake.
No comments:
Post a Comment