Raisi Jose Mujica wa Uruguay
Hebu fikiria viongozi wa Tanzania (raisi, mawaziri na wabunge)
wangekuwa wazalendo kama Jose Mujica, natumai kwa utajiri uliopo
Tanzania basi wananchi wangekuwa na maisha mazuri na Tanzania ingekuwa
mbali sana.
Raisi Jose Mujica wa Uruguay (Amerika kusini) mwenye umri wa miaka
77 tokea alipochaguliwa kuwa raisi mwaka 2009 bado anaishi kwenye nyumba
yake. Alipoulizwa na watangazaji wa BBC waliomtembelea nyumbani kwake
ni kwanini hataki kuishi Ikulu, raisi Mujica alisema kuwa hahitaji
kuishi kwenye jumba kubwa.
Hii ndio nyumba anayomiliki na kuishi raisi wa Uruguay na amekataa
kujengewa nyumba nyingine mpya. Water supply ya nyumbani kwake ni kutoka
kwenye kisima alichochimba mwenyewe na kuunganisha hadi ndani. Nyumba
inalindwa na askari na kakataa kuwekewa fence kubwa kuzunguka shamba
lake ili kuimalisha ulinzi wa nyumba.
Gari analomiliki raisi ni Vokswagen Beatle yenye umri wa miaka 25
(toleo la mwaka 1987), pamoja na tractor analotumia kwa kilimo.
Raisi Mujica alishinda uchaguzi wa uraisi mwaka 2009. Asilimia 90,
equivalent to $12,000 (£7,500) ya mshahara wake kwa mwezi hupeleka
kwenye charity na kusaidia jamii masikini (hasa za mashambani) kwa
shule, hospitals na huduma nyinginezo za jamii. Mawaziri wake
walimwambia kuwa atumia pesa yake nyingi mno kusaidia watu, yeye anajibu
kuwa hiyo asilimia 10 (£485) inayosalia kwa mwezi inamtosha kuishi
maisha mazuri, hahitaji pesa nyingi na wala mavazi mengi. Salio hilo la
mshahara wake ni sawa karibu na mshahara wa watu wa kawaida nchini
Uruguay.
Raisi Mujica na tractor yake kwenye shughuli za kilimo.
Raisi Mujica anamiliki nyumba mbili za kawaida na moja iko shambani
anakoishi, tractor ajili ya shamba na gari aina ya Volkswagen Beatle kwa
matumizi yake na mkewe. Alipoulizwa na BBC team nyumbani kwake kuwa
anajisikiaje kuitwa na wananchi wake kuwa yeye ni raisi masikini
duniani, yeye anajibu kuwa yeye sio masikini na wala hajisikii kuwa
masikini. Asema kila mtu ana uhuru wa kuishi maisha anayotaka, anaishi
vyema kwa hivi alivyo navyo. Na ameishi maisha haya maishani mwake mote.
Aongeza kuwa masikini ni wale wanao fanya kazi nyingi kujaribu kuishi
maisha makubwa ya kifahari na wakipata hawaridhiki wanataka tena na tena
na tena, utajiri wa mali hauleti furaha, utajiri ni kuridhika na vile
ulivyo navyo.
Raisi Mujica anapokuwa likizo hutumia muda wake mwingi na mkewe
kwenye shughuli za kilimo hasa cha maua. Na pia hujumuika na wana kijiji
eneo ambalo anaishi kwa miaka mingi katika shughuli za kilimo na
maendeleo iwe kutengeza mitaro ya maji au kujumuika na wazee.
Raisi Mujica akibeba dumu la maji shambani mwake
Raisi Mujica akiwa na mbwa wake mwenye miguu mitatu anayeitwa Manuella
No comments:
Post a Comment