Wang Liyang akijizalisha mwenyewe ndani ya basi |
Thursday, December 20, 2012 2:22 AM Katika tukio ambalo limewashangaza wengi, mwanamke mmoja nchini Chini alijizalisha mwenyewe bila ya msaada wa mtu yeyote wakati akiwa ndani ya basi pamoja na abiria wengine akienda hospitali. |
|||||||||||||||||||
Mwanamke
huyo aliyetajwa kwa jina la Wang Liyang mwenye umri wa miaka 39, akiwa
amekaa kwenye basi pembeni ya mtoto wake wa kiume mwenye umri wa miaka
mitatu, alifunua nguo zake na kujizalisha mwenyewe mtoto wa kiume huku
mtoto wake mwingine wa kiume akiangalia bila ya kujua kinachoendelea. Taarifa zilisema kuwa bi Liying akiwa na mwanae wa miaka mitatu, alipanda basi kwenye kwenye mji wa Chengdu, Sichuan akienda hospitali ili akafanyiwe uchunguzi zaidi kutokana na maumivu ya tumbo yaliyokuwa yakimsumbua. Video ya ulinzi ndani ya basi hilo ilimuonyesha mwanamama huyo akifunua nguo zake na kuanza kujizalisha mwenyewe na kisha kuanza kumsafisha mtoto wake huyo kabla ya kumbinua kichwa chini miguu juu na kumchapa kidogo matakoni ili alie na hivyo kuzifungua vizuri njia zake za hewa ili aweze kupumua vizuri. Video hiyo iliwaonyesha baadhi ya abiria wakijitokeza na kumpa nguo za kumfanya ajihifadhi zaidi yeye na mwanae mchanga. Dereva wa basi hilo aliongeza spidi ili kumwahisha hospitali lakini kabla hawajafika ilitokea ambulansi ambayo ilimwahisha mama huyo hospitali. Taarifa zaidi ziliongeza kuwa mama huyo na mtoto wake mchanga wa kiume mwenye uzito wa kilo 3.2 wote walikuwa na afya njema na wanaendelea vizuri. |
Saturday, December 22, 2012
VIDEO - Mwanamke Ajizalisha Mwenyewe Ndani ya Basi
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment