Wednesday, January 9, 2013

Hii imechangia sana kuharibu maisha na kukatisha matarajio ya vijana wengi wa Kitanzania,ni kweli?

Mdau unatambua ni kitu gani hicho? Katika vitu ambavyo vimepelekea vijana wengi wa Kitanzania na Dunia kwa kujumla kupoteza uelekeo wa maisha yao na hiki kipo. Vijana wengi wamekua wakipoteza muelekeo wa maisha yao kutoka na madhara ya matumizi ya hiki kitu.

Kipindi cha nyuma ilikua ni adimu sana kuona au kusikia harufu ya hii kitu. Lkn siku hizi hadi watoto wadogo wanaifahamu harufu yake. Kwani inatumia sehemu yoyote bila uoga wowote. Si ajabu mtu kukaa sebuleni kwako ukahisi harufu ya hii kitu. Pia ni kawaida sana siku hizi mwanao(mtoto) kukwambia "Baba nahisi harufu ya nanihii....".

Tatizo linakuja pale hata wale wanaotakiwa kupiga marufuku matumizi ya hii kitu, na wao kutumia mia. Mbaya zaidi kumekua na tuhuma juu ya matumizi ya hii kitu hata kwa baadhi ya viongozi. Ilishawahi semekana kuwa hata baadhi ya wabunge wetu wanatumia hii kitu.

No comments:

Post a Comment