Mshiriki wa mchezo wa pikipiki akiwa hewani huku chini kukiwa na mtoto mdogo.Bahati nzuri mtoto hakuangukiwa na pikipiki hiyo.
NA DUNSTAN SHEKIDELE,MOROGORO.KATIKA hatua ya kusheherekea sikuu ya mwaka mpya wakati wa mji wa Morogoro jana walishuhudia uhondo wa michezo ya pikipiki uliofanyika ndani ya uwanja wa saba saba huku michezo hiyo ikigubikwa na hatari nyingi.
Moja ya hatari hizo ni pale mshiriki maonyesho hayo Bw Abdul Juma aliponusurika kumuangukia mtoto aliyekuwa jirani na uwanja huo wa saba saba akishuhudia michezo hiyo.
Mbali na tukio hilo pia mshiriki huo nalinusulika kifo baada ya pikipiki, yake kumtupa alipokuwa hewani akionyesha michezo hiyo.
Katika onyesho hilo Mtandao huu haukushuhudia muongozo au ulinzi wowote wa jeshi la polisi,jambo ambalo limechangia kwa kiasi kikubwa kutokea kwa hatari hilo.
Akizungumza na Mtandao huu mratibu wa oneysho hilo Bw Athuman Mahita alidai kwamba kila mwaka anaanda onesho hilo mara mbili.
" Hii ni mara ya pili mara ya kwanza nilianda siku ya sikuu ya ldd na mara ya pili ni leo sikuu ya mwaka mpya"alisema Mahita kwa kujiamini.
kwa sasa mchezo huo umevuta hisia za wakazi wengi wa mji wa Morogoro ambao jana walioneka kufulika kwa wingi kushuhudia mchezo huo kwa kulipa kiingilio cha shilingi elfu moja.
No comments:
Post a Comment