Saturday, January 26, 2013

Wizi na ubakaji wahamia Saint John's Dodoma baada ya IFM


 




Wanachuo wakiwa wameshika mabango ya kushinikiza ulinzi katika chuo cha St. John
Usiku wa kuamkia leo wanafunzi watatu wa chuo cha 'Saint John's' Dodoma walivamiwa na wezi na kuibiwa laptops 3, camera 1,fedha Tsh. 120,000 na hatimaye mmoja wao kubakwa.Wanafunzi hao wamepanga nje ya chuo hicho na wanaishi wasichana pekee katika nyumba hiyo waliopanga.

Akizungumza na tulonge.com kwa njia ya simu, afisa uhusiano wa chuo hicho Bw. Karim Meshack amethibitisha tukio hilo kutokea na mkuu wa mkoa wa Dodoma Dk. Rehema Nchimbi aliitisha kikao cha dharura. Maamuzi yaliyo fikiwa katika kikao hicho ni pamoja na kuanzisha kituo cha polisi eneo la chuo hicho pamoja na kuweka taa eneo la karibu na chuo hicho kwani kuna giza sana.

No comments:

Post a Comment