POLISI Wa Afrika Kusini wamewatia mbaroni watu 19 kwa tuhuma za
kuhusika na upangaji wa njama kwa ajili ya kuipindua Serikali ya
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Taarifa iliyotolewa na Mamlaka ya Taifa ya Uendeshaji Mashtaka
ya Kongo ilisema kuwa watu hao walikuwa na lengo la kupata mafunzo
maalumu ya kijeshi ili kuipindua Serikali ya sasa inayoongozwa na Rais
Joseph Kabila. Kwa mujibu wa taarifa hiyo iliongeza kuwa hadi sasa
hakuna taarifa yoyote iliyoashiria kuwepo kwa uhusiano kati ya watu hao
19 waliotiwa mbaroni na kundi la waasi la Machi 23.
Watuhumiwa hao 19 ambao hadi leo hakukuwa na taarifa kamili juu
ya majina yao wanatarajiwa kufikishwa mahakamani leo katika Mji wa
Pretoria.
Msemaji wa Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Lambert
Mende alisema kuwa viongozi wa nchi hiyo walikuwa na ufahamu juu ya
harakati zilizokuwa zikiendelea nje ya nchi dhidi ya Serikali.
Watu hao 19 walitiwa mbaroni katika Mkoa wa Limpopo, Kaskazini mwa Afrika Kusini.
Awali wapiganaji wa Kundi la M23 wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo walisisitiza kwamba, hawataondoka katika Mji wa Goma wanaoudhibiti licha ya kutakiwa kufanya hivyo na marais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Rwanda na Uganda.
Awali wapiganaji wa Kundi la M23 wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo walisisitiza kwamba, hawataondoka katika Mji wa Goma wanaoudhibiti licha ya kutakiwa kufanya hivyo na marais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Rwanda na Uganda.
M23 Walitoa wito wa kuachia ngazi kwa Rais Joseph Kabila wa
nchi hiyo wakisisitiza kwamba, hakushinda katika uchaguzi uliofanyika
Novemba mwaka jana.
Wachambuzi wa mambo wanaamini kuwa, kukimbia kwa vikosi vya
Serikali mjini Goma baada ya kuzidiwa na mashambulio ya waasi
kumeteteresha nafasi ya Rais Kabila.
No comments:
Post a Comment