Tatizo la uwezo wa kufanya tendo la ndoa linazidi kukua miongoni wa
wanandoa na wapenzi wengi. Takwimu za kitafiti zinaonyesha kuwa karibu
ndoa 4 kati ya 10 zenye umri wa miaka 3 na kuendelea zinakabiliana na
tatizo hili. Aidha wanaume 6 kati ya 10 wanatajwa kulalamikia upungufu
wa nguvu za kiume na kuacha idadi ya wanawake wanaokabiliwa na tatizo
hilo kwa mujibu wa uchunguzi kubaki na asilimia 13.
Pamoja na
matatizo mengine kutajwa kuchangia upungufu wa nguvu za kiume na kushuka
kwa msisimko wa tendo miongoni mwa wanandoa, uchunguzi umeonesha kuwa
utumiaji holela wa vyakula hasa vyenye mafuta ni moja kati ya sababu
zinazochangia kwa kasi tatizo hili.
Kwa kuzingatia hilo, watafiti wa
masuala ya uhusiano wa kimapenzi wamebaini aina kumi ya vyakula ambavyo
vina uwezo wa kumuongezea mtu nguvu ya kufanya tendo la ndoa. Vyakula
hivyo ni hivi vifuatavyo:
PILIPILI
Pilipili zilizocheshwa
zimetajwa kuwa na uwezo wa kusaidia msukumo wa usambazaji damu mwilini,
ambao kwa kiasi kikubwa ndiyo unaoweza kumfanya mtu akawa na hisia kali
za kimapenzi. Kwa msingi huo, ni vema kwa wale wanaokabiliwa tatizo la
uwezo wa kufanya mapenzi wakatumia pilipili si kwa wingi bali kwa
kiwango stahili, ili waamshe hisia zao.
PARACHICHI
Aina
nyingine ya chakula ambacho husaidia kuongeza uwezo wa mtu kufanya tendo
la ndoa ni Parachichi. Tunda hili linauwezo mkubwa wa kuzalisha
vitamini E ambayo husaidia katika uzalishaji wa homoni. Inatajwa kuwa
watu wanaotumia tunda hili kwa wingi huwana msisimko mkali wa kimapenzi
na kwa upande wa wanawake husaidia kuongeza majimaji yenye utelezi
sehemu za siri na hivyo kuzuia uwezekano wa kuchubuka wakati wa
kujamiiana.
NDIZI
Wakati unafikiria uwezo wa kufanya vema
tendo la ndoa unatakiwa kuwaza juu ya uimara wa misuli ya mwili ambayo
inatajwa kuwa ni sehemu kuu na yenye muhimu katika kujamiiana. Kwa
msingi huo ulaji wa ndizi mbivu unatajwa kusaidia kujenga misuli mwilini
na kumfanya mtu aweze kuwa hodari katika tendo la ndoa.
CHOKOLETI
Ulaji wa Chokoleti huongeza uchangamfu mwilini na, hivyo kumuwezesha
mtu anayeshiriki tendo la ndoa kuwa na mguso sahihi kwenye fikra zake,
jambo litakalomuwezesha kupokea hisia za mapenzi kwa urahisi zaidi ya
mtu ambaye anakwenda kwenye uwanja wa sita kwa sita akiwa mchovu wa
mawazo.
CHAZA NA PWEZA
Aina hizi za samaki zinazovuliwa
baharini huwa na madini ya zink na chumvi ambayo yanatajwa kusaidia
uzalisha wa vichocheo vinavyohamasisha msisimko wa mwili wakati wa tendo
la ndoa.
POMEGRANATE
Ni aina fulani ya matunda mekundu
yanayofananana na apple. Haya yatajwa kusaidia kuamsha mishipa ya fahamu
na kuweka mawasiliano sahihi ya mwili na hivyo kumuongezea mtu uwezo
kwa kufanya tendo la ndoa kwa hamasa kubwa.
MVINYO MWEKUNDU
Mvivyo mwenyekundu unatajwa kuwa na uwezo wa kuuchangamsha mwili na
kuongeza msukumo wa damu, kiasi cha kumuondolea mtu uchovu kabla na
baada ya tendo la ndoa, hivyo ni muhimu kunywewa hasa na wale ambao
wanasumbuliwa na tatizo la kushindwa kurudia tendo.
MBEGU ZA MATUNDA
Mchangayiko wa mbegu mbalimbali za matunda, mfano tikiti, maboga
husaidia kuondoa ACID mwilini na kumfanya mtu ajione ni mwenye afya
njema.
VANILLA
Vanila husaidia kuamasha hamasa mwili.Mwisho
wa aina hizi za vyakula ni TIKITI MAJI ambalo linatajwa kuwa na
virutubisho vingi vyenye uwezo wa kuusaidia mwili kuwa na nguvu za
kutosha kufanya tendo la ndoa.
No comments:
Post a Comment