Tuesday, May 7, 2013

Kilimanjaro: Mzee wa miaka 49 amlawiti mwanafunzi wa darasa la tano


Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Baltazar Panklas Swai (49) mkazi wa Kitasha Mengeni wilyani Rombo mkoani Kilimanajro anashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoani hapa kwa kosa la kumlawiti mwanafunzi wa darasa la tano mwenye matatizo ya akili.
Kwa mujibu wa Taarifa ya Jeshi la Polisi iliyotolewa kwa waandishi habari inasema  tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia Aprili 25 katika kijiji cha Aleni Chini.
Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro limesema kitendo hico kimemsababishia maumivi makali katika sehemu zake siri.
Mwanafunzi aliyefanyiwa kitendo hicho cha kinyama (14) ni wa darasa la tano katika Shule ya Msingi Mengeni wilayani humo.

Imebainikia kwamba mwanafunzi huyo ni mgonjwa akili na mbinu iliyotumika kumkamata mzee huyo ni ushirikiano wa wananchi wa kijiji hicho kwa usimamizi wa Mwenyekiti Correntini Masawe.

Mashuhuda wa tukio hilo wamesema mtuhumiwa pia ni mhalifu sugu kwani alishawahi kufungwa gerezani miaka ya nyuma kutokana na matukio ya kihalifu  huku wakilaani kitendo alichokifanya mtuhumiwa na kuvitaka vyombo vya dola kuchukua mkondo wake.

Mwandishi: YOHANA GERVAS
Mhariri: JOHNSON JABIR
jaizmelaleo.blogspot.com

No comments:

Post a Comment