WAKATI hali ikizidi kuwa tetea Mkaoni Mtwara kufutia Mapigano
yaliyoanza jana Mkoani humo Rais Kikwete amevunja ukimwa wake na kutoa
amri wahusika wakuu wa tukio hilo kusakwa mara moja.
Akizungumza katika eneo la Kizota,
Dodoma wakati wa kuweka jiwe la
msingi la ujenzi wa Barabara ya Dodoma kwenda Iringa, Rais Kikwete
alisema wote waliohusika na vurugu hizo watasakwa na kuchukuliwa hatua
kali.
Rais Kikwete alisema rasilimali inayopatikana mahali popote pale nchini inatakiwa kutumiwa na Watanzania wote... “Hivi watu wa Nyarugusu
wadai dhahabu ya pale au kinachopatikana Chalinze basi kisitumiwe na
watu wa Morogoro! Hivi tutakuwa na taifa kweli?,” alihoji kwa ukali Rais Kikwete.
Rais Kikwete alisisitiza kuwa Serikali itawasaka wale wote
wanaoongoza vurugu hizo na watawajibishwa kwa makosa hayo... “Tutawasaka
hawa watu na viongozi wao hata kama wana mapembe kiasi gani, tutayakata.”
Kwa upande wake Waziri Muhongo Waziri
wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo akisoma taarifa ya
mapato na matumizi ya Wizara yake alisema mradi wa kusafirisha gesi
kutoka mkoani Mtwara kwenda Dar es Salaam, umeanza kwa kasi na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda atakwenda huko wiki ijayo kuweka jiwe la msingi.
Akiwasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Nishati na Madini jana, Waziri Muhongo alisema:
“Mradi wa kujenga bomba la gesi uko palepale na unaendelea kwa kasi
na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ataenda kuweka jiwe la msingi wiki lijalo.”
No comments:
Post a Comment