Vita
iliyoanzishwa na Mr II aka Joseph Mbilinyi mbunge wa Mbeya kupitia
tiketi ya chama pinzani cha CHADEMA juu ya unyonyaji na unyanyasaji wa
wasanii wa mziki wa kizazi kipya huenda ikachukua sura mpya baada ya
kundi la vinega kuungana na Lady Jay Dee katika vita yake dhidi ya
Clouds FM.Vijana waliotoa maoni yao katika baadhi ya mitaa ya jiji la
Dar Es Salaam ambako ndiko makao makuu ya Clouds FM na mahali ambako
kuna wasanii wengi zaidi walisema huenda kundi la vinega likaungana na
Lady Jay Dee na kufungua Radio yao ambayo itakua ni kama revenge kwa
adui zao.
Hivi karibuni zimefanyika juhudi kubwa kunusuru wasanii kutumbukia
katika umaskini wa kutupwa dhidi ya makampuni ya simu kunyonya kazi zao
na upande wa pili baadhi ya radio ambazo zinaonesha upendeleo ,
unyanyasaji na unyonyaji wa wazi kwa kazi za wasanii.Clouds FM hivi
karibuni imeshutumiwa na Lady Jay Dee kuendesha kampeni za kumuua
kisanii ambapo pia imewalipa baadhi ya wasanii ambao walitakiwa
kuhudhulia show ya Lady JayDee ili wasitokee katika shoo hiyo.Jamii
haipendezwi na vita hii japo serikali imeonekana kufumba macho na
kujifanya haioni kinachoendelea.Tuko pamoja katika kuona haki,usawa na
amani vinatendeka.Mungu Ibariki Tanzania
No comments:
Post a Comment