THE WORST VALENTINE’S DAY...SEHEMU YA PILI

Alinitazama machoni na ndipo nilipoona macho yake
yakiwa mekundi na miale ya moto ilioneka na kwenye macho yake,,meno miwili
marefu yalichomoza mdomoni kwake na ile hali ilizidi kunitisha na nilitamani
nife ili nisione yaliyokuwa yanatokea,,alinisogelea na kunishika na kisha
akanisemesha kwa lugha ya kiarabu lakini sikuelewa aliirudia tena ile lugha na
wakati huu akinisogelea kwa karibu,,nilitetemeka sana na kwa muda mfupi
nilikuwa tayari nimekonda lakini sikuweza kusogea wala kupiga kelele, wakati
huo wale wengine walikuwa bado wamejifunika usoni na vitambaa vyeusi na
walikuwa wameinama kama wanasujudu,,,haya yote yalikuwa maajabu
kwangu,,,taratibu nilianza kuona ule ukuta wa nyumba ukirudi kama mwanzo na
umeme ukarudi nilitazama pale sebuleni palikuwa pakubwa na idadi ya watu
waliokuwa pale walikuwa ni zaidi ya hamsini na kulikuwa na boksi kubwa nyuma
yao kama vile la friji,,hapo Jamshid aliendelea kunitazama na kuniongelesha kwa
ile lugha ya kiarabu hata ivyo sikujibu kwakuwa sikuielewa na hapo alibadili
lugha na kuanza kuongea Kiswahili;
“Asalam aleyku”alinisalim mara hii kwa salam ambayo
nayo sikuweza kuijibu,,
“Jina langu naitwa jini Shamsu, naishi katika kilindi
cha maji ndani ya bahani ya hindi nyumbani kwetu ni Nungwi, mbele yako kuna
majini tofauti zaidi ya 50 ila niwatambulishe kwa majina wakuu wangu,,ATHA huyu
ni mkuu wangu, ndiye mungu wa kiarabu wa kuabudu sanamu,,yupo TARAKADHURU jini
lililompa baba yako mali kwa masharti akakiuka,,yupo jini AL-RAHAB aliyekukatia
umeme wakati tunakuja,,yupo jini ABADI ambaye ndio yeye na kundi lake
waliohusika kuvamia nyumba yenu na kumbaka mama yako mpaka kufa,,yupo jini FARK
na majani mengine”. Ilikuwa sauti ya Jamshid ikiongea hayo yote ambayo kwangu mimi
sikuyaelewa na hapo akili yangu ilihama na kurudi miaka mingi nyuma wakati wale
majambazi wameivamia nyumba yetu,,,ilikuwa ni majira ya saa nane usiku ambapo
nilikia sauti ya baba na mama wakipiga kelele nikashtuka na muda mfupi mbele
nikatoka mpaka kwenye korido na ndipo nilipokamatwa na kupelekwa moja kwamoja
mpaka pale walipowekwa wazazi wangu na mimi nikafungwa pamoja nao,,mama yangu
alichukuliwa na kuvuliwa nguo mbele yangu na baba na kisha walianza kumuingilia
mmoja baada ya mwingine,,,alilia kwa uchungu sana lakini hakuna ambalo
tungeweza kufanya nakumbuka yale majambazi yalimgeukia baba na kuanza
kumsemesha kwa lugha ambayo hata ivyo sikuielewa na baba aliwajibu huku
akionekana kuzidi kuomba msamaha,,kwakuwa akili yangu ilikuwa ndogo sikuwaza
ile ni lugha gani na kwanini mambo yote yalitokea kwa haraka,,,nakumbuka kesho
yake asubuhi mama alifariki lakini usiku ule baada ya wale majambazi kuondoka
nilimsihi baba tumpeleke hospitali lakini alikataa na badala yake alimpigia
simu mtu nisiyemfahamu na kuongea nae kwa lugha ileile ile ambayo wale watu
waliongea nae na sasa ndo napata akili kuwa lugha ile ilikuwa ni kiarab,,siku
moja baada ya mazishi ya mama nakumbuka vizuri kuwa baba aliniita na kuni na
kunikalisha chini na maongezi yetu yalianza kwa yeye kunipa mlolongo mrefu wa
mambo ambayo hata hivyo sikuelewa maana hakuwa wazi;
“Binti yangu mama yako amefariki na hatuna la kufanya
juu ya hilo,,wewe una umri mdogo lakini kuanzia hivi sasa unatakiwa ujifunze
kujitegemea na kuongoza biashara zangu na miradi mingine” hiyo ilikuwa sauti ya
baba yangu ikinipa taarifa na hapo ilikuwa ni siku moja kabla ya kifo chake
“baba tupo wote mimi sidhani kama nitaweza kufanya
hayo”nilimuambia kwa sauti ya upole lakini nilishangaa baba alivyoamka na sauti
ya ukali
“utaweza na ni lazima uweze,,usiseme tupo wote,,” hiyo
ilikuwa sauti ya baba yangu ikinipa taarifa na hapo ilikuwa ni siku moja kabla
ya kifo chake
“baba tupo wote mimi sidhani kama nitaweza kufanya
hayo”nilimuambia kwa sauti ya upole lakini nilishangaa baba alivyoamka na sauti
ya ukali
“utaweza na ni lazima uweze,,usiseme tupo wote,,you are
only you,,am dead already (uko peke yako, mimi nimeshakufa
tayari)”..Nilishangazwa na taarifa hii lakini zaidi sikutilia maanani maneno ya
baba kwakuwa nilijua ni msongo wa mawazo kwa kifo cha mke wake, lakini
alinyanyuka pale na kusimama pembeni akachukua simu yake ya mkononi na kuanza
kupiga simu na hapo nilimsikia akiongea na mtu kwa lugha ya kifaransa;
“la cargaison est arrivѐѐ?” (Mzigo uliwasili?) Ilikuwa sauti kavu ya mzee ikiuliza na baada ya
upande wa pili kujibu nilisikia tena akimsemesha kuashirika kuwa tayari
walishakubaliana.
“Venez chez moi maintenant” (Njoo nyumbani kwangu sasa
hivi),,baada ya hapo baba alibonyeza teza vitufe vya simu yake na akaiweka tena
sikioni na sasa alikuwa akiongea na Rorbahcho rafiki yake wakijerumani
aliyekuwa akiishi Tanzania ambaye ndiye niliyekuwa nikimchukulia kama baba
yangu mdogo kwakuwa sikuwahi kumuona ndugu ya baba yangu,,,waliongea kwa sauti
ya chini lakini niliweza kumsikia baba akimueleza jambo na kwakuwa nilielewa
japo ni kidogo nilimuelewa;
“Ich konnte jeden Tag ab heute sterben” (ninaweza kufa
siku yoyote kuanzia leo) hili lilikuwa kati ya maneno machache sana ambayo
niliyasikia katika yale maongezi ambayo baba aliongea na Mzee Rorbahcho
lilinishtua na kuniumiza ila sikuelewa chochote kilichokuwa kikiendelea pale
niliendelea kumsikiliza akiongea na nilibahatika kusikia maneno mengine na
kiasi cha pesa kilichonishtua;
“make 200,000/= pfund auf meiner tochter-konto
übertragen”(hamisha paundi 200,000 taslim kwenda kwenye akaunti ya binti
yangu),,fedha hii ilikuwa ni sawa na shilingi za kitanzania milioni mia
tano,,nilitaka kumuuliza baba nini kilikuwa kinaendelea lakini sikupata mda wa
kufanya ivyo kwani baada ya yeye kumaliza kuongea na simu hiyo alimpigia simu
Samah Jiraz ambaye ni binti mwenye asili ya kiarab na mda si mrefu niliona
akiingia na gari yake nyeusi aina ya Cadillac,,Samah alikuwa ni mwanasheria wa
familia yetu na baada ya yeye kufika kwa haraka niliitwa ndani na makabidhiano
ya mali yalianza,,mambo yalikwenda haraka sana na sikuweza kuuliza chochote
zaidi ya kuweka sahihi kwenye lundo la makaratasi yaliyokuwa pale mezani,,na
baada ya muda mfupi tulimaliza na Samah aliambiwa anipeleke kwenye kila sehemu
ambayo tumeweka sahihi makatasi yake,,,niliingia kwenye gari ya Samah na muda
mfupi mbeleni tuliingia kiwanda cha Maji ya kunywa cha MORIS FOOD INDUSTRIES na
hapo alikusanya wafanyakazi wote na kunitangaza kama mmiliki wa kiwanda
hicho,,,hakuna aliyehoji na sikuwa naelewa nini kinaendelea bado,,,niliingia
kwenye gari na moja kwa moja nilipelekwa maeneo mengine mengi na mida ya saa
saba tuliingia kwenye nyumba kubwa ambapo ndani nilikutana na mwanamke mrembo
aliyevaa baibui ya rangi ya dhahabu na Samah alinitambulisha kuwa yule aliitwa
Maysa ndiye aliyemsaidia baba yangu kupata uraia wa Tanzania kipindi alipoingia
nchini akitokea Rwanda enzi izo akiwa kijana,,alinifahamisha kuwa Maysa alikuwa
ni Msaidizi wa balozi wa Oman nchini Tanzania lakini hata hivyo sikuelewa
kwanini tuko pale,,,waliniingiza ndania na mara hiyo Maysa aliniambia nisiogope
chochote na akaja mbele yangu na chupa ya juice na kuniwekea nilipoinywa
nilitapika lakini alichoniambia ni kuwa sasa naweza kujitegemea yote yalitokea
haraka na hakuna muda wa kuuliza swali nilikuwa kama nimepigwa na butwaa lakini
baada ya kunywa ile juice nilipata nguvu za ghafla na woga uliniishia.
*****
“Faith” nilishtuka toka kwenye dimbwi la mawazo
lililonifanya nisahau kilichokua mbele yangu.
“Abee” niliitika kwa sauti ya mshtuko iliyojaa woga na
kilio,,Jamshid alinyanya mikono yake kama aliyekuwa akiagiza kitu na hapo wale
watu wote walikaa pande mbili na katikati yao kukatokea sufuria kubwa lenye
maji ya moto yanayochemka.
“Leo ni siku ya wapendanayo na ni siku ya kutimiza
maagano,,ni siku ya malipizi ni siku ya adhabu kwa wote waliosaliti ufalme wa
majani,,leo ni siku ya sherehe na leo ni siku ya kunywa damu,,leo ni siku ya
kufunuliwa kwako na siku ya kujua ukweli unaouma” aliongea Jamshid na hapo
aligeuka na kuongea na wale waliokuwa wameketi pale ambapo ukuta ulichanika na
wao kuingia,,,aliwasemesha kwa lugha ya kidachi ambayo na mimi ghafla
nilijikuta nikiifahamu;
“Brengen dat verrader hier” (mleteni yule msaliti hapa)
hapo waliondoka wale jamaa kupitia ile kona ya ukuta na hapo walirudi na mtu
kwenye kiti chenye matairi kupitia pale kwenye ule ukuta na alikuwa
amefunikwa,,baada ya kumfikisha pale aliwanyanyua wengine na kuwaambia tena kwa
lugha ile ile ila muda huu alisema kamleteni yule Malaya,,,baada ya hawa kutoka
aliingizwa mtu mwingine akiwa na hali kama ile ya yule wa kwanza na hapo
walifunuliwa vile vitambaa,sikuamini nilichokiona,,,alikuwa ni baba yangu na
mama yangu wote wakiwa hai,,walikuwa wamekonda na walionekana wadhoofu kupita
maelezo nililia kwa uchungu mkubwa na kutaka kuwafata lakini sikuweza kunyanyua
mguu pale nilipokuwa,,nililia nikimuita mama na baba lakini haikusaidia mana
wao pia machozi yaliwatoka na walionekana wakitaka kuongea lakini hali
waliyokuwa nayo sauti haikuweza kutoka,,,hapo niliisikia tena sauti ya Jamshid
ikiita na hapo wasichana wawili waembo waliamka na kutoa vitambaa vyao na
mikononi walikuwa na mapanga mawili marefu yaliyokuwa yaking’aa kuonyesha kuwa
yanilikuwa makali kama wembe,,,nilifuta machozi na kuwatazama usoni sikuamini
kuwa wale walikuwa MAYSA NA SAMAH…
UNATAKA
KUJUA KILICHOENDELEA????UMEUPENDA MKASA HUU NA HADITHI HII?? Hahaaa tuendelee
kuwa pamoja
No comments:
Post a Comment