Mkurugenzi wa Benchmark Productions Limited, ambao ndio waandaaji wa EBSS Madam Ritha Poulsen amekanusha habari ya kumpandisha kizimbani mwanamuziki wa Bongo fleva Ney wa Mitego kwa kosa la kumsema Ritha kuwa hawapatii hela washindi wa BSS(Bongo Star Search) pamoja na maneno mengine ambayo yapo kwenye wimbo wa Salaam zao wa mwanamuziki huyo.Pia ilisemekana angemdai fidia ya Tsh. mil 500 kwaajili ya kumdhalilisha
Akizungumza na Clouds Fm, Ritha alisema hana mpango wa kumshitaki msanii huyo kwani hana muda wa kufanya jambo hilo. Hata hivyo Ney hana uwezo wa kulipa fedha hiyo. Muda kwake ni mali hivyo hawezi kuupoteza kwa jambo hilo. Alipoulizwa kama anaweza kumruhusu Ney aje kuimba kwenye fainali za EBSS za mwaka huu, Ritha alijibu anaweza kabisa kumruhusu na atapenda aimbe wimbo huo huo wa Salam zao.
Aliongeza kwa kusema Ney atakua ametumia fursa hiyo ili kujulikana zaidi kwa watu, na ni kweli amefanikiwa sababu hata yeye (Ritha) amemjua vizuri.
Katika wimbo wa Salaam zao, Ney alimponda mshindi wa EBSS 2012 Walter Chilambo kuwa ana maisha magumu japo alitangazwa kushinda mil 50. Kutokana na hili Ney alihitimisha kwa kudai hela za washindi wa BSS huwa haziwafikii walengwa.
Pia katika wimbo huo amegusia watu mbalimbali maarufu wakiwemo Rais, wabunge, wanasiasa na watu wengine maarufu.
No comments:
Post a Comment