Wednesday, September 25, 2013

Bomu lalilipuliwa usiku Darajani Zanzibar


NewsImages/6989966.jpg
Tuesday, September 24, 2013 10:41 AM
KISIWA cha Zanzibar kimeingiawa na hofu nyingine ukiachia mbali ile ya tindikali ambapo juzi watu wasiojulikana wameanza kurusha milipuko inayoidhaniwa kuwa ni mabomu katika moja ya maduka lililopo maeneo ya Darajani

Mara baada ya kurushwa kwa kitu hicho kilichodaiwa kilikuwa na umbo la Soseji moshi mkali mkubwa ulianza kufuka kutokea eneo kulikorushwa kitu hicho

Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi mkoa wa Mjini Magharibi, Mkadam Khamis Mkadam alisema kuwa, bomu hilo lilirushwa katika duka la Sahara Store lililopo Darajani na kuangukia katika kreti lililokuwa na chupa ya soda.

Alisema mbele ya vyombo vya habari kuwa, tukio hilo lilitokea majira ya saa 8:30 usiku wa kuamkia jana

Alisema katika eneo hilo kulikuwa na walinzi na mmoja kati yao aliyemtaja kwa jina la Amour Kassim alikwenda kuokota kitu hicho bila kujua na poshi ukaanza kufuka nay eye akaarusha kitu hicho na ndipo kikasikika kishindo na moshi kuongezeka

Alisema wamegundua kuwa lilikuwa bomu baada ya kuonekana ungaunga mweupe

Kamanda huyo alisisitiza kuwa wananchi wawe makini eneo hilo na kuongeza ulinzi umeimarishwa eneo hilo na hakuna mtu aliyejeruhiwa wala hakuna wahalifu waliokamatwa kuhusiana na tukio hilo na upelelezi wa kna unaendelea

Hata hivyo Kamanda Mkadam aliwataka wananchi watoe ushirikiano kwa jeshi la polisi ikiwemo na kutoa taarifa hilo na zitakazosaidia kuwakamata wahusika

Mji wa Zanzibar kwa sasa wakazi wake wamekuwa wakiishi kwa tahadhari baada ya kasi ya kumwagiana tindikali ikizidi kwa kasi visiwani humo

Hadi sasa matukio yasiyopungua matano ya viongozi wa dini na watu wengine kumwagiwa tindikali

No comments:

Post a Comment