Friday, October 18, 2013

Diamond Platinumz hapa umekosea


'Fuck the police', hiki ndicho kilichoandikwa kwenye 'vest' ya Diamond kama inavyoonekana pichani.Sina hakika kama hiki kitu si sawa, au ni ushamba wangu unanisumbua. Diamond ni mmoja kati ya wasanii wa Tanzania ambao husisitiza heshima katika kazi ya muziki ili ufanikiwe zaidi. Hicho kilichoandikwa katika 'vest' aliyoivaa ndo heshima yenyewe? na kina leta picha gani katika jamii? Anaonekana hivi kwenye video ya wimbo mpya wa msanii Dully Sykes uitwao 'Kabinti Special'. Kuna uwezekano mkubwa video hii ikatazamwa na watu wengi ndani na nje ya Tanzania. Sielewi watazamaji watamuweka kwenye kundi gani. Unadhani ile kampeni ya kuwashawishi wazee waamini muziki wa kizazi kipya si wakihuni itafanikiwa kirahisi kwa mwenendo huu?

No comments:

Post a Comment