Friday, October 18, 2013

Mtoto wa msanii Afande Sele ambaye uwezo wake darasani umemfanya aanze kidato cha kwanza akiwa na miaka 11

 
Afande Sele kulia, akiwa na mwanae Tunda
Wale wafuatiliaji wa muziki wa kizazi kipya 'Bongo Fleva' watakua wanamfahamu vizuri Tunda ambaye ni mtoto wa mfalme wa Rhymes Tanzania, Afande Sele. Tunda alipozaliwa takribani miaka 11 iliyopita, Afande Sele alikua akimtaja sana katika nyimbo zake na alipokua akihojiwa.Hii ilipelekea jina la Tunda kukaa vichwani mwa Watanzania hasa mashabiki wa Afande Sele.
Tunda huyu sasa ni binti wa miaka 11, na sasa yupo Kidato cha kwanza. Ni binti mwenye uwezo mzuri darasani. Alifanya mtihani wa Darasa la 7 kipindi alipokua darasa la 6 na kufanya vizuri. Hii ni kwa mujibu wa baba yake kama alivyoeleza hapo chini kupitia ukurasa wake wa facebook.

Hapa chini ni familia nzima ya Afande
 
Toka kushoto ni Tunda,Sanaa,Afande na Mkewe. Mambo ya nyota ya kijani umeyaona mdau?

No comments:

Post a Comment