UFUSKA NDANI YA BONGO MOVIE....WASANII HULIPWA NA KUHONGWA MAGARI ILI KUTOA "PENZI" BILA KINGA...
KINACHOONEKANA
kwa sasa Bongo ni ugumu wa serikali kupambana na vita dhidi ya
maambukizi ya Virusi vya Ukimwi baada ya jamii kushindwa kubadilika na
kuona ugonjwa huo ni wa kawaida kama ilivyo kukohoa au kichwa kugonga.Hilo
limedhihirika baada ya juzi chanzo chetu cha habari kupasha kwamba,
baadhi ya wafanyabiashara na wabunge wameingia ‘kazi’ ya kuwanasa mastaa
wa kike Bongo, hasa waigizaji wa filamu.
Kwa
mujibu wa chanzo hicho, wafanyabiashara maarufu wa jijini Dar na baadhi
ya waheshimiwa wabunge wamekuwa wakiwaibukia mastaa wanapokuwa kambini
wakirekodi filamu na kuwahonga fedha nyingi sanjari na kuwanunulia
magari ya kifahari ya kutembelea.
Inadaiwa
wanachofanya baadhi ya mastaa, hasa wakiwa kambini, hupiga picha chafu
wakiamini zina mvuto na kuzitundika BBM kwenye simu zao ambapo
wafanyabiashara na wabunge hao wanapoziona huweweseka na kuanza msako wa
kuwapata.
Chanzo kilisema: “Zamani mapedeshee ndiyo walikuwa
wanaongoza kwa kuwachukua mastaa wa kike kwa kutumia picha za mitandaoni
na kwenye magazeti, siku hizi mastaa wenyewe wamewashtukia, hawawataki
mapedeshee, wanasema fedha zao ni za msimu.
“Siku
hizi mastaa wakiwa kambini hupiga picha za hasarahasara na kuzitupia
BBM, wafanyabiashara na wabunge wakiziona wanakimbilia kupanga foleni
kwenye mahoteli ambayo mastaa hao wamepiga kambi.”
Aidha,
chanzo kikasema kuwa baadhi ya wafanyabiashara huhonga kuanzia shilingi
1,000,000 hadi 5,000,000 kama staa ana jina kubwa.
“Kama
staa ana jina kubwa, anaweza kuhongwa kuanzia milioni moja hadi tano,
kama ni supastaa kama Wema, Wolper, Odama, Rose Ndauka hawa wanaweza
kuhongwa hata magari ya kifahari,”kilisema chanzo hicho.
Chanzo
kikasema kuwa, mbaya zaidi wanaume hao wamekuwa wakigoma kufanya
mapenzi kwa kutumia kinga (kondom) kwa madai kwamba, hawawezi kuhonga
pesa nyingi halafu kitandani wakatumia kondom kwani wanakosa raha.
“Kinachouma
zaidi ni kwamba, hao wanaume wakiwachukua mastaa hadi chumbani
wanakataa kutumia kondom, madai yao pesa wanazohonga ni ndefu (nyingi)
kwa hiyo ni afadhali wafaidi, wanasahau kwamba Ukimwi upo.
“Kwa
sababu ya tamaa ya pesa, dada zetu (mastaa) wanashindwa kuwa na msimamo
wa kutumia kondom. Anaweza kukataa sana, lakini mheshimiwa anaahidi
kumnunulia gari, hapo ndipo masharti yanalegezwa,”kilisema chanzo.
Chanzo
kikasema kumekuwa na vilio na kusaga meno kwa baadhi ya mastaa kwani
wanaponunuliwa magari, kadi zinakaa kwa wanaume hao, baadaye
wanawanyang’anya.
“Mbaya zaidi,
wapo mastaa waliwahi kushawishika na kutoa penzi bila kinga kwa ahadi ya
kununuliwa gari, waliponunuliwa hawakupewa kadi ya kumiliki, baadaye
wakanyang’anywa,” chanzo kilitoboa.
Baadhi ya mastaa
waliozungumza na paparazi wetu walikiri kuwepo kwa wanaume wenye tabia
hiyo, lakini kila mmoja akasema yeye haijamtokea.
Wolper: “Ni
kweli, wapo wanaume wanabembeleza sana kutotumia kondom na kuahidi
fedha au gari, lakini kama staa anakubaliana na ombi hilo ni
kujiangamiza, Ukimwi unaua. Ila mimi sijawahi kukutana na mwanume wa
hivyo, kwanza nilishasema ndani ya gari natembea na kondom.”
Jack wa Chuz: “Wewee,
uamuzi wa kufanya hivyo ni wa mtu mwenyewe na umri wangu huu nikubali
kufanya mapenzi bila kinga kwa sababu ya gari? Kwani gari kitu gani
bwana.”
Nisha: “Mh!
Nimewahi kusikia kuna wasanii waliingia kwenye mtego huo na sasa
wanajuta maana hawana uhakika na afya zao, kwenda kupima wanaogopa,
magari walishanyang’anywa, mimi aku!”
Flora Mvungi: “Mimi siwezi kusema kitu maana nina wangu, kama ni gari au pesa ananipa yeye, pole yao ambao hawajajipanga hadi leo.”
Aidha,
chanzo kilisema kuwa, maeneo hatari ya kufanyika kwa michezo hiyo ni
hoteli kubwa ambazo wasanii hupiga kambi kwa ajili ya kurekodi filamu.