Friday, December 6, 2013

Ahukumiwa miaka 10 jela kwa kuzini na MBUZI

Kushoto ni mbuzi aliyetendewa ukatili huo na Bwana Katana kulia wakiwa mahakamani
Katana Kitsao Gona (28) amehukumiwa miaka 10 jela baada ya kukutwa na hatia ya kufanya mapenzi na mbuzi huko Malindi Kenya. Tukio hili lilitokea tarehe 25 Novemba 2013. Shuhuda wa tukio alieleza kuwa alishangazwa kuona nguo zikiwa zimetundikwa kwenye mti alipokua akipinda karibu na kichaka ambapo tukio hilo lilitokea. Alipojaribu kufuatilia zaidi alimuona Bwana Katana akiwa uchi na akifanya mapenzi na Mbuzi aliyekua amefungwa kwenye mti kichakani. Ndipo alipoamua kutoa taarifa kwa mmiliki wa mbuzi huyo na kuja kumkamata Bw Katana na kumpeleka mbele ya vyombo vya dola.

Vipimo vilidhihirisha kuwa ni kweli mbuzi huyo alitendewa ukatili huo na mtuhumiwa. Sehemu za siri za mbuzi huyo zilikua zikitoka damu.

Licha ya mshitakiwa kujitetea kuwa ana mke ambaye ni mlemavu wa miguu na anamtegemea yeye lakini Mahakama haikutilia maanani utetezi wake na kumuhukumu kifungo cha miaka 10 jela.

No comments:

Post a Comment