Wednesday, February 5, 2014

Dodoma:Askari polisi 5 wamefariki papo hapo baada ya gari yao Corolla kugongana na Basi la Mohamed trans


Askari polisi 5 wamefariki papo hapo baada ya gari yao Corolla kugongana na Basi la Mohamed trans huko Dodoma.

Askari watano wa jeshi la polisi kituo cha polisi wilaya ya Kongwa wamefariki papo hapo katika ajali ya barabarani baada ya gari dogo aina ya Toyota Corolla walilokuwa wakisafiria kutoka Dodoma manispaa kwenda wilayani Kongwa kugongana uso kwa uso na basi la abiria la kampun i ya Mohamed trans lililokuwa linatoka jijini Dar es Salaam kwenda mkoani Dodoma katika kijiji cha Mtumba kilichopo nje kidogo ya mji wa Dodoma.

Akizungumzia ajali hiyo iliyotokea majira ya saa sita na robo usiku wa kuamkia Jumamosi hii kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma kamishna msaidizi mwandamizi wa polisi David Misime amesema chanzo cha ajali hiyo ni iliyolihusisha gari dogo aina ya Toyota Corolla lenye namba za usajili T 770 ABT na basi aina ya Scania lenye namba za usajili T 997 AVW ni mwendokasi wa madereva wa magari yote mawili .

Kamanda misime amewataja askari waliofariki katika ajali hiyo kuwa ni Adolf Sila, Evarist Bukombe, Patric Mahinyila, Jacline Tesha na Jema Luvinga wote wakazi wa Kongwa ambapo amesema msiba huo ni pigo kubwa kwa jeshgi la polisi mkoa wa Dodoma.

Hata hivyo mara baada ya kutokea ajali hiyo dereva wa basi aliyetambulika kwa jina la Juma Mohamed mkazi wa jijini Mwanza alikimbia na kutokomea kusikojulikana ambapo hadi hivi sasa anatafutwa na jeshi la polisi mkoa wa Dodoma ili aweze kufikishwa katika vyombo vya sheria.

No comments:

Post a Comment