Mtu
mmoja anaesadikiwa kuwa ni jambazi ambaye hakufahamika jina
anayekadiliwa kuwa na umri wa miaka 25 ameuwawa kwa kupigwa mawe kisha
kuchomwa moto na mwingine kunusurika kuuwawa.
Tukio
hilo limetokea jana alfajiri katika kijiji cha Shibula kata ya
Bugongwa wilayani Ilemela Mkoani Mwanza kufuatia tukio la wizi lilotokea
usiku wa kuamkia jana katika mtaa wa Nyamwilolelwa ambapo pikipiki
moja na paneli ya solar ziliibiwa.
Katibu
wa Sungusungu katika kijiji cha Shibula John Mashalia amesema kuwa
kufuatia tukio hilo waliamua kuweka ulinzi shirikishi kuzunguka vijiji
vyote na ndipo walipokutana na kijana huyo aliyeuwawa akiwa na kijana
mwingine aliyefahamika kwa jina la Edward Aloyce ambao walidai
wanatafuta pikipiki iliyopotea.
Mashalia
ameongeza kuwa kata ya Bugongwa imekuwa na matukio ya ujambazi mara kwa
mara ikiwa ni pamoja na vitendo vya ubakaji kwa watoto na wanawake.
Kwa
upande wake mkaguzi msaidizi wa jeshi la polisi Joyce Kotecha amewataka
wananchi wa kata hiyo kuacha kujichulia sheria mkononi na kwamba
wawasiliane na uongozi wa kata yanapotokea matatizo ya namna hiyo.
Kijana aliyeuawa kwa kuchomwa moto
Vijana wa sungusungu wakiwa katika mlango wa duka ambapo kijana mwingine aliyenusurika alifungiwa kungoja polisi waje
Hii ni pikipiki ambayo vijana hao walienda nayo eneo la tukio
Polisi wakiwsili eneo la tukio
Polisi wakipanga jinsi ya kumtoa mtuhumiwa huyo
Ambulance ikiandaliwa kupakia maiti ya kijana huyo….Mwili wa kijana huyo ukiwa chini baada ya moto kuzimika
Polisi wakipakia pikipiki iliyokutwa eneo la tukio
Machela ikiandaliwa kuupakia mwili huo….
Polisi wakikagua makoti ambayo kijana aliyenusurika alikuwa ameyavaa
Mwananchi akiburudika na kilimanjaro ya moto baada ya tukio hilo…..
Msaidizi wa polisi Inspecta Joyce Kotecha akiwasihi wananchi watulie ili sheria ichukue mkondo wake
Polisi wakiwa getini kwa maandalizi ya kumtoa kijana aliyenusurika…..
Kijana aliyenusurika aitwaye Mangi akitolewa ndani ya duka kwa ulinzi mkali na kupakiwa kwenye gari…
Kijana Mangi akiwa ndani ya gari, pembeni yake ni maiti ya mwenzake…..
No comments:
Post a Comment