Mkazi
wa Mtaa wa Lagos, Wazo Mivumoni, Msitu wa Pande jijini Dar es Salaam,
Nuru Makala ‘Baba Eliza’ (42) Jumatano iliyopita alikumbwa na majanga
baada ya mwanaume aliyejulikana kwa jina la Yusuf Ally ‘Mgosi wa Ndima’
kudai amemfumania Baba Eliza akiwa na mkewe ambaye jina halikupatikana.
Tafrani hiyo ilijiri usiku wa Jumatano iliyopita, Juni 18, mwaka huu kwenye nyumba yake iliyopo Mtaa wa Lagos, Msitu wa Pande.
Akizungumzia
tukio hilo mbele ya wanahabari waliokuwa eneo hilo wakisaka
habari, Yusuf Ally ambaye ni mume wa mwanamke aliyefumaniwa
alisema:
“Nilikuwa
katika harakati za kumchunguza mke wangu kinyemela kwa siku nyingi kama
anachepuka, nikabaini kuna mawasiliano yenye shaka kati yake na huyo
jirani yangu.
“Nilipomuuliza
mke wangu alikiri, akasema amekuwa akimwambia jirani yangu kwamba
haiwezekani lakini jamaa anakomaa tu anamwambia wakutane, tena wakutane
humu ndani.
“Ndipo
nilipoamua kumuandaa mke wangu kwa mtego amwambie jamaa kuwa leo (siku
ya tukio) sitakuwepo na sitarudi ili kumpa nafasi jamaa kuja kujinafasi.
Baada ya kukamilisha mtego niliwasiliana na kamanda wa sungusungu wa
eneo hilo, Kapteni Makumba na kumuelezea kinagaubaga.
“Kapteni
Makumba aliwaandaa vijana wake ambapo kuanzia mishale ya saa mbili
usiku walijibanza kwenye kichaka kilichopo mbele ya nyumba huku akifanya
mawasiliano na mimi.”
Yusuf aliendelea kudai kuwa, ilipotimu saa tano usiku kukiwa kumetulia, Baba Eliza alionekana akikaribia nyumba ya jirani yake huyo kwa hatua za kunyata na kuangalia kulia na kushoto kisha akazama ndani huku mkononi akiwa ameshika kifurushi kilichobainika baadaye kwamba kilikuwa na machungwa kadhaa.
Alisema
muda mfupi baada ya kuingia, sungusungu mmoja alikwenda kujibanza
kwenye dirisha la chumba na kupiga chabo kilichokuwa kikiendelea ambapo
alimshuhudia Baba Eliza akichojoa nguo chapchapu tayari kwa mtanange,
sungusungu huyo akawatonya wenzake.
Yusuf
akazidi kusema kwamba wote walitoka kichakani na kwenda kuvamia
chumbani ambapo walimkuta mkewe aliyekuwa bado hajaanza kuvua nguo kwa
sababu alijua majanga yatatokea muda si mrefu akiwa anajiandaa kufanya
hivyo kiaina.
Baada
ya hali kuwa shwari, Kamanda wa Sungusungu, Kapteni Makumba alianza
kumsomea mashitaka jirani huyo aliyekuwa mtupu muda huo mbaye hakuwa na
la kusema zaidi ya kuomba radhi na kumtupia lawama ibilisi kwamba ndiye
aliyemshawishi na haikuwa amri yake.
Sungusungu walimtaka Baba Eliza kumlipa fidia ya shilingi milioni moja mwenye mke kwa kitendo cha kumdhalilishia ndoa yake.
Read more: http://mchimbuzi.blogspot.com/2014/06/aibu-jamaa-anusurika-kunyofolewa-jicho.html#ixzz39yc5TWGg
No comments:
Post a Comment