Thursday, July 19, 2012

NDOA YENYE FURAHA HUDUMISHA UPENDO WA DHATI!

Ndoa ni nini? Ndoa ni muungano wa mwanaume na mwanamke unaokubalika kiutamaduni na kidini ambao unatarajiwa kudumu, kuwapa haki sawa za kijinsia na kutosheleza majukumu mengine ya kijamii. Katika ndoa kuna uhalali wa watoto.
Pamoja na tafasiri hiyo ya ndoa, watu wengi siku hizi wamekuwa wakiishi maisha ya ndoa kama fasheni hali ambayo imekuwa ikishusha hadhi ya ndoa. Si jambo la ajabu kusikia ndoa iliyofungwa wiki moja iliyopita imevunjika baada ya wanandani hao kutwangana makonde.
Katika ndoa kuna matabaka mawili. Tabaka la kwanza ni kwa wanandoa kufurahia ndoa yao na tabaka la pili ni la wanandoa kuijutia ndoa yao. Hakika ndoa inaraha sana na nitendo la heshima mbele za Mungu.
Hivi ulishawahi kujiuliza ni kwa nini siku ya harusi wanandoa wote huwa na furaha? Na je, furaha hiyo baadaye hupotelea wapi? Hakuna mwanandoa yeyote ambaye huwaza kama siku moja yeye na mwenzi wake wanaweza kukorofishana na kutukanana matuzi mazito ambayo hugeuka kuwa sumu ndani ya ndoa yao.
Siku ya harusi kila mmoja huisubiri kwa shauku kubwa na kuona siku kama haziendi ili wanandoa hao wawe pamoja katika jahazi la ndoa ya maisha. Lakini mambo hubadirika kwa baadhi ya wanandoa pindi wanapoanza maisha ya pamoja. Kabla sijaendelea naomba kukuuliza wewe uliyendani ya ndoa, je ulishawahi kujiuliza ni kwanini furaha mliyokuwa nayo wakati hamjaoana leo hii haipo hivyo? Kumbuka mara nyingi penzi linalotolewa wakati wa uchumba huwa lina mbinu nyingi za kusomana tabia na kila mmoja hupenda kuficha tambia yake mbaya aliyonayo. Ni suala gumu kigodo kwa wanandoa ambao kila mmoja amekulia katika malezi tofauti kukaa na kujenga tabia moja. Wakati watu wanapokuwa katika hatua ya uchumba hushindwa kusomana vizuri tabia zao kutokana na umbali walionao. Kwa sababu kila mmoja anakuwa kwao ama kwake hali ambayo hutoa muda mwingi wa kumkumbuka mpenzi wake.
 MR ABDALLAH KUNDAVI A.K.A MAN PHILO..AKIWA NA MKE WAKE....

No comments:

Post a Comment