Zoezi la sensa ya watu na makazi kwenye mkoa wa Kigoma lilipata ugumu
kutokana na waumini wa dini ya kiislamu wanaopinga kuhesabiwa
kukimbilia misikitini hivyo kutofikiwa na makarani waandikishaji.
Mkuu wa wilaya Kigoma Ramadhani Maneno amesema kwenye pitapita yao
kufanya tathmini wamekutana na ugumu huo na tayari wameanza kuufanyia
kazi, maeneo ambayo wamegundua tatizo hilo ni pamoja na Mwandiga na
Katonga ambapo licha ya kutaka kuongea na viongozi wa misikiti hiyo,
wameshindwa kupata ushirikiano wowote hivyo amesema kamati ya ulinzi na
usalama inatarajia kukaa kujadili ili kuona hatua za kuchukua.
Amekaririwa akisema “kuna baadhi ya viongozi wa kiislam wameshawishi
waislam wenzao kwenda kulala misikitini ili kusiwe na nafasi tena kwa
makarani wa sensa kuingia misikitini, nilipojaribu kwenda kwenye msikiti
wa Mwandiga kujaribu kushawishi niongee na viongozi wao, sikufanikiwa”
Mwandishi Fadhili Abdallah anasema Mkuu huyo wa wilaya amethibitisha
jumla ya kaya 40 kati ya 64 kwenye kijiji cha Bubango kata ya Bitale
Kigoma Vijijini, zimekataa kuandikishwa kufuatia maelekezo ya viongozi
wa kaya hizo.
No comments:
Post a Comment