Tuesday, August 14, 2012

KITAA KINALALAMIKA VIDEO YANGU HAIKUTENDEWA HAKI SASA NAISHOOT UPYA "TUNDA MAN"


Tunda Man jana majira ya jioni alikuwa anafanya video yake nyingine ambayo ni kama anairudia baada ya ile ya kwanza kutengenezwa na Adam Juma wa Visual Lab. Video hiyo sio nyingine basi ni hii inayoitwa DEMU SIO na hizi picha nilimpiga jana wakati akishoot na kampuni nyingine ya utengenezaji video inayoitwa APEX chini ya Dir Pablo.
Nilipomuuliza kwanini unairudia kushoot video hii tena alinijibu kuwa kitaani kama wananchi hawajaielewa video aliyoshoot Adam so kama inamgharimu kuirudia tena video hiyo ili kuchange mapishi na kuona kama je mashabiki zake watalalamika tena au la.
Nilipofika eneo hilo alilokuwa akishoot maeneo ya Kijitonyama Sayansi aisee nilikutana na vyombo hatariiiii nazungumzia wasichana ambao wataonekana wakicheza katika video hiyo, stay tune ujionee mwenyeweeeee

No comments:

Post a Comment