Mimi kama mimi kwa mtazamo wangu naona mapenzi ya
siri yana ukomo wake marafiki zangu.Unapokuwa unapenda mapenzi ya siri
sana, unampa wakati mgumu mwenzako. Ni rahisi kufikiria kwamba, unafanya
hivyo kwa kuwa ama hujiamini au una mtu mwingine. Weka mambo hadharani.
Mtambulishe mwenzi wako kwa marafiki zako. Jiamini, unapokutana na mtu
uliyesoma naye zamani au kuishi naye sehemu moja, mwambie kwamba
uliyenaye ni mwenzako na unatarajia kuingia naye kwenye ndoa.
Kufichaficha kunaondoa utamu wa mapenzi. Kunazidisha maswali ambayo
hayana majibu. Kama yapo ni huyo mwenzako kujijibu mwenyewe. Kwa
kawaida, hatajipa majibu mazuri. Yatakuwa ya kinyume – yenye tafsiri
mbaya. Kwamba yawezekana hutaki kumtambulisha kwa kuwa una mtu mwingine.
Je, ni kweli? Kama ndivyo huna sababu ya kumpotezea muda mwenzako. Kama
si kweli, basi amka. Gundua kwamba ulikuwa unafanya makosa na uanze
ukurasa mpya.
Ni mtazamo tuu,hata wewe waweza kuwa na mtazamo wako.
Ni mtazamo tuu,hata wewe waweza kuwa na mtazamo wako.
No comments:
Post a Comment