Monday, September 17, 2012

Akamatwa na maiti ya mtoto ndani ya begi...NIGERIA

Tukio hili lilitokea jana huko Gwarimpa, Abuja, Nigeria. Kijana ambaye jina lake limehifadhiwa alipanda kwenye basi na begi ambalo hakutaka kondakta alishike pale alipoombwa. Hapo ndipo vurugu ilipoanza, kwani kuna sehemu maalumu ya kuweka mizigo lakini mtuhumiwa hakutaka kumpa kondakta begi lake ili liwekwe sehemu hiyo maalumu.
Kondakta na abiria waliamua kumnyang'anya begi kwa nguvu kijana huyo na baada ya kulifungua walikuta maiti ya mtoto wa kiume ndani. Kijana huyo anashikiliwa na polisi kwa maelezo zaidi.

No comments:

Post a Comment