Wiki hii nilikutana na wasomaji wangu kadhaa kama ilivyo ada yangu
kuwashauri watu ana kwa ana kila Jumapili kwa wale waliohitaji kuongea
nami kwa kina, miongoni mwa watu nilioongea nao niligundua kuwa, wengi
wapo katika utumwa wa mapenzi na walikuwa wanapoteza muda wao bila
kujua! Kwa kutambua jambo hilo, nimelazimika kuwaletea mada hii ili
usije jiingiza kwenye uhusiano ambao utakupotezea muda na kama upo
katika uhusiano huo huna budi kujinasua. Sasa endelea kujifunza:-
Usiipe nafasi hofu Nyote mnapaswa kuwa na hisia zenye afya ili kujenga
uhusiano wenye mafanikio. Kwa mfano, siyo dalili nzuri kama unakuwa
kwenye uhusiano kwa sababu tu unahofu kuwa mpweke.
Ni vibaya pia kwa mwanaume wako kusema anaupenda mchezo fulani kama
anavyokupenda! Au ukiwa na msongo wa mawazo, usinase kwenye mtego wa
mapenzi kwa kudhani unaweza kuwa tiba. Ni vizuri zaidi kutafuta mwanaume
ambaye hahitaji utabibu.
Chunga mwendo wako
Jihadhari na chunga mwenendo wako kwani wanaume huwa makini na
hushangazwa zaidi wakati wapenzi wao wanapokuwa wanafanya mambo ya
ajabu. Unapozungumza naye muangalie usoni siyo sakafuni.
Usimuulize maswali mengi kuhusu kazi yake, ingawa ni muhimu kujua
anafanya kazi gani, kwani anaweza kuwa jambazi ati! Anaweza kudhani
unataka kumchuna tu.
Kama utashindwa kuchunga tabia yako, usishangae kama kukutana kwenu siku
ya kwanza kunakuwa ndio mwisho wenu na usipojiangalia utajikuta tayari
umemfunulia!
Kufanana huleta mafanikio
Hii haimaanishi unapaswa kuolewa na ndugu au mzazi wako, la hasha!
Lakini unapoanza uhusiano na mtu, hakikisha unamfahamu kwanza kwa undani
na jiulize mara mbili kama kuna vitu ambavyo mnalingana.
Fikiria kuhusu uhangaikaji wake katika maisha (hata kama hana uwezo
mkubwa kifedha, je, anajuhudi za kuzisaka hizo fedha ama la?), ujuzi na
hata mapenzi ya dhati.
Na fikiria sana kama malengo katika maisha yenu yanarandana. Nyote
mnapaswa kukubaliana kuhusu athari pia za ndoa na kukabiliana nazo kama
kuwa na watoto, kuishi kwenye nyumba ya mbavu za mbwa au hekalu.
Vipo vitu unavyoweza kuvitambua kwa kukutana kwenu mara moja au mara mbili, na nyote mnapaswa kuwa wazi.
Toa upinzani
Mfanyie kila uwezalo mpenzi wako ili atambue kwamba unampenda, lakini
usitake kuchukulia dalili zake za kuridhika na wewe mapema ndizo
zikupumbaze na kumganda.
Hapa sizungumziii kanuni – usisite kuijibu simu yake atakapokupigia au
kwenda kukutana naye atakapokuita, hata hivyo, epuka kukutana naye
sehemu ya uficho kama chumbani, lakini usijenge maisha yako kumzunguka
yeye na wala usimlazimishe akakuelezea hisia zake.
Hakikisha kwamba yeye ni nyongeza katika maisha yako na siyo muhimili wa maisha yako.
Usiwe domokaya
Najua wengi wenu mna mambo mengi ambayo mnaweza kuyazungumza, lakini
yahifadhi mengine kwa ajili ya siku nyingine. Wanaume hupenda kusikia
habari mpya kila mnapokutana.
Wanawake wanapaswa kufikiria kuhusu hadithi mbili au tatu kali ambazo
wanaweza kuzungumza wanapokuwa kwenye miadi, lakini wasivuke mpaka na
kuanza kuzungumza mambo yanayowahusu wenyewe!
Usinune
Wanaume wengi huwa wanalalamika kwamba hupata wakati mgumu zaidi
wanapokuwa na wapenzi wao, hasa katika siku ya kwanza ambapo hushindwa
hata kuwabusu, kama huyo uliyenaye ndiye chaguo lako, basi usiwe mgumu,
tabasamu na kama atakubusu usikwepeshe uso wako.
Itaendelea wiki ijayo, unayaonaje makala haya? Nimuvuzishie maoni yako kwa kutumia simu: 0715-888887 au brazatk@yahoo.com au kutembelea http://mwakilaga.blogspot.com kurasa pepe namba moja inayokupa nafasi
ya kujifunza kuhusu mapenzi na kukupatia meseji kali za mapenzi,
marafiki na wachumba. Kwa wale wanaohitaji ushauri wasisite kuwasiliana
nami.
No comments:
Post a Comment