- Mapenzi kitu ajabu, yakutia bumbuwazi
Yakufanya uwe bubu, kujibu huwa huwezi
Shubiri kwako zabibu, na vitamu huviwezi. - Wamkuta kaemewa, asemayo hayajuwi
Aumba akiumbuwa, aona maruwiruwi
Vigumu kumuopowa, na kwa ngisi kumvuwi. - Hukumbuka ya zamani, yote walofanyiana
Nyumbani barabarani, ayaona kama jana
Akili yake ya nyani, aruka inagongana. - Wangoja nyota ya jaha, kutwa wewe unahaha
Mawazo yako silaha, akukwaaye usaha
Usifanyiwe msaha, waugeuza karaha. - Kalelewa kaleleka, utani kwake ni mwiko
Njiani yeye na kaka, hapokei mualiko
Ghadhabu zake za paka, hapendi maziko.
Sunday, September 9, 2012
MASHAIRI YA MAPENZI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment