“Huduma haziendi kama kawaida, hatujui ni nani
aliyevumisha habari hiyo, cha kusikitisha hata baadhi ya vyombo vya habari vimeripoti,
kwamba tukio hilo lipo kama vile waliliona, huu ni uongo, iwe wafu au wazima,
sijaona watu kama hao hapa,” alisema Dk Malima.
Mitandao ya kijamii ilidiriki hata kuweka picha ambazo
nyingi zikionesha kama zimechezewa zikidai kuwa watu wapo hospitali ya Temeke.
Baadhi ya watu walidai kuwaona wawili hao
waliong’ang’aniana walidai, walikumbwa na mkasa huo katika nyumba ya kulala
wageni na mwanamke, ndiye sababu ya tukio hilo baada ya kutegewa na mumewe.
“Hilo tego ni la mwanamke, yaani ukimwona yule dada
huwezi kuamini, mimi nimemwona maana ninafanyakazi huko hospitalini, ni aibu,
wamefunikwa kwa shuka la gesti, suala hilo si la kutibiwa hospitalini ni mpaka
mumewe aje ndio watengane,” alisema msichana mmoja.
Baadhi ya watu nje ya hospitali walisikika wakisema
mmoja kati ya watu hao amekufa, wengine wakidai wote wawili wamekufa kwa
shinikizo la damu, lakini walipohojiwa zaidi walishindwa kutoa uthibitisho wa
maelezo yao.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Temeke, David Misime
(aliyehamishiwa Dodoma), akizungumza kwa simu, alisema ni uvumi usio na ukweli.
No comments:
Post a Comment