Wanaume wa shoka (FFU) walilazimika kufanya kazi ya ziada kutawanya wananchi waliozunguka kwa maelfu hospitali hiyo wakitaka kushuhudia uvumi ulizagaa kwa fasti kama umeme kwamba kuna mke wa mtu na mume wa mtu wamenasiasa katika uzinzi.
Inadaiwa kwamba watu hao wawili walinasiasa wakiwa wanafanya mapenzi wakifanya mapenzi kwenye nyumba moja ya kulala wageni iliyoko maeneo ya Mbagala, Dar es Salaam mapema leo.
Kwa mujibu wa watu waliodai kushuhudia tukio hilo wamesema kwamba baada ya juhudi za kujinasua kushindikana, wawili waliomba msaada na kupelekwa katika Hospitali ya Temeke kwa ajili ya kujaribu kutenganishwa, lakini daktari wa hospitali hiyo amekana kuwapo watu hao.
Aidha baadhi ya watu walisema kwamba watu hao walikuwa wamefichwa nyuma ya mochari huku wengine wakisema wameshakufa na wengine wakisema kuokoa hospitali huyo na uwezekano wa kutokea hamaniko la watu ambalo linaweza kuumiza wengi zaidi.
Watu wanaojidai kuona mambo hospitalini hapo walidai kushuhudia gari moja aina ya Toyota Canter likiingia hospitalini hapo majira ya Saa 4 asubuhi likiwa limewabeba wapenzi hao walionasiana huku wakiwa wamefunikwa shuka la nyumba ya wageni .
No comments:
Post a Comment