Saturday, December 22, 2012





VIDEO - Ukisikia Mwanamke Aliyedata Basi Ndiye Huyu...

NewsImages/6612078.jpg
Ukisikia kuna mademu wamedata basi huyu ni mmoja wao
Wednesday, September 26, 2012 1:30 AM
Marekani kuna wanawake wengi ambao wanajifanya wamewehuka na kufanya vitu mbalimbali vya aibu bila kujali watu waliowazunguka lakini kali ya yote aliitoa mwanamke huyu ambaye alijikojolea ndani ya treni na kisha kuamua kuoga kabisa ndani ya treni.
Mwanamke huyo akiwa ndani ya treni hiyo ya jijini New York alianza kwa kudai amebanwa na mkojo kabla ya kuamua kuliachia kojo ndani ya treni.

Kama haitoshi mwanamke huyo alidai lazima aoge baada kujichafua kwa mkojo. Mwanamke huyo alitoa dumu la maji toka kwenye begi lake pamoja na sabuni na kuanza kuoga mbele ya abiria waliojazana ndani ya treni ambao walibaki midomo wazi hawajui la kufanya zaidi ya kumuacha mwanamke huyo aendelee na zoezi lake la kuoga.

Video ya dakika tano ikimuonyesha mwanamke huyo akijikojolea na baadae akioga iliwekwa kwenye YouTube wiki hii na kuwa gumzo kwenye mitandao mbali mbali duniani.

Angalia VIDEO hiyo chini.


                                                                                                                                                    VIDEO - VIDEO - Ukisikia Mwanamke Aliyedata Basi Ndiye Huyu...








No comments:

Post a Comment