Tuesday, January 22, 2013

Ajinyonga na kufa akidai anakwenda kwa Yesu

MWANAUME mmoja mkazi wa mitaa ya Vumilia mjini Kahama, Bw.Mayala Mwagala 58 amejinyonga hadi kufa chumbani kwake kwa madai kuwa anakwenda kwa Yesu.

Marehemu huyo anadaiwa kujinyonga kwa kutumia kama ya katani juzi usiku baada ya kukutwa akiwa mening'inia kwenye kenchi chumbani kwake alikokuwa amepanga.

Jeshi la Polisi wilayani Kahama limethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo lilisema kuwa Dada wa marehemu, Bi. Josephina Mwagala alisema kaka yake alikuwa naye siku moja kabla ya kujinyonga kazini kwake kwenye grosale ya Sadala katika mazungumzo ya kidugu na aliachana saa nne usiku.

Bi. Mwagala alisema wakati akiwa nae marehemu kaka yake alikuwa akimtamkia kuwa saa sita usiku itakuwa mwisho wa maisha yake duniani atakwenda kwa Yesu. Alisema wakati anaongea maneno hayo hakuwa anamjali na wala hakuweza kumuuliza kwa nini anasema hivyo kuwa usiku huo itakuwa mwisho wa maisha yake na anakwenda kwa Yesu.

Bi.Mwagala alisema kuwa kaka yake huyo hakumueleza kama kuna tatizo lolote linalomkabili na familia yake. Alisema baada ya kuachana naye yeye alikwenda kwake na mke wake alikuwa amemwacha shamba katika kijiji cha Burungwa wilayani hapa na kwamba anashanga muda wa saa tano mchana alifuatwa na wapangaji wenzake na kumueleza kuwa kaka yake amekufa kwa kujinyonga.

No comments:

Post a Comment