Katibu
wa Baraza la Filamu Tanzania (TAFF), Wilson Makubi, amethibitisha
kutokea kwa msiba wa Sajuki, ambaye alikuwa akisubiriwa apate nafuu ili
Serikali ya Tanzania igharamie safari na matibabu yake nchini India
MSANII
nyota wa filamu Tanzania, Juma Kilowoko, ‘Sajuki,’ amefariki dunia saa
moja asubuhi ya leo, katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alikokuwa
akitibiwa.
Sajuki
aalifikishwa hospitalini hapo mwishoni mwa Desemba 2012, alikofikishwa
akitokea Amana, alikokuwa akipata matibabu mbaada ya kuanguka jukwaani
jijini Arusha, alipopanda kutaka kusalimia mashabiki wake ikiwa ni
harakati za kutafuta fedha michango ya pesa za kumpeleka tena India
kupata matibabu.
Katibu
wa Baraza la Filamu Tanzania (TAFF), Wilson Makubi, amethibitisha
kutokea kwa msiba wa Sajuki, ambaye alikuwa akisubiriwa apate nafuu ili
Serikali ya Tanzania igharamie safari na matibabu yake nchini India.
Makubi
alisema kuwa, maandalizi ya msiba huo yatatangazwa baada ya wahusika na
wadau kukukutana, huku akiwataka mashabiki wa sanaa na msanii huyo kwa
ujumla kuwa wavumilivu katika kipindi hiki cha maandalizi ya mazishio
yake.
Kabla
na baada ya kuifika India kwa matibabu, Sajuki aligunduliwa kuwa na
ugonjwa wa uvimbe pembeni ya ini, ambapo aliporejea alionekana kuimarika
kiafya, kabla ya kuanza kuugua tena.
Kifo
cha Sajuki kinafanya muendelezo wa vifo vya wasanii nguli wa filamu na
muziki ulioanzia mwaka uliopita, ambapo wakali kama Steven Kanumba, John
Maganga, Mlopelo, Sharo Milionea, Mariam Khamis ‘Paka Mapepe’
walifariki kwa nyakati tofauti kutokana na maradhi na ajali.
Mchakato
wa mazishi ya Sajuki unafanyika Tabata, jijini Dar es Salaam.
MUNGU
ailaze ROHO ya marehemu SAJUKI mahali pema PEPONI. Ameen.

No comments:
Post a Comment