Rais Kikwete akitangaza matokeo ya sensa 2012
Rais Kikwete ametangaza matokeao ya Sensa ya mwaka 2012 katika
Viwanja vya mnazi mmoja jana. Jumla ya watanzania wote ni 44,929,002
ambapo kati ya idadi hiyo Tanzania Bara ni 43,625,434 na Zanzibar ni
1,303,568.Katika kuhakikisha watanzania wengi wanayapata matokeo haya, ujumbe umekuwa ukitumwa kwenye simu za viganjani za watanzania ikionesha imetoka kwa Rais Kikwete huku ikitaja idadi ya watanzania kwa ujumla na kubainisha idadi ya Bara na Visiwani pia.
Idadi ya watu nchini imeongezeka kutoka watu milioni 34.4 kwa takwimu za Sensa ya mwaka 2002 hadi kufikia watu milioni 44, 929,002 takwimu za Sensa ya mwaka 2012 ambapo kwa kipindi cha miaka kumi kumekuwepo na ongezeko la watu zaidi ya milioni 10.
No comments:
Post a Comment