Wednesday, January 16, 2013

Huyu ndiye mgombea kiti cha Urais Jamhuri ya Czech mwenye 'tattoo' 90% ya mwili wake.

Vladimir Franz ni mmoja kati ya wagombea tisa wa kiti cha Urais Jamhuri ya Czech ambaye asilimia 90 ya mwili wake umechorwa 'tattoo'. Pamoja na hilo kura za maoni zimempa 11.4% ya kura zote ambapo amekua ni mgombea wa tatu kati ya wagombea hao 9. Franz mwenye umri wa miaka 53 ana shahada ya sheria, ni profesa wa fani ya maigizo pia ni mchoraji.
Franz alisema kuwa 'tattoo' ni jambo lake binafsi, halina uhusiano na kugombea kiti cha Urais. Pia ushindani wa kiti cha Urais siyo shindano la urembo.

No comments:

Post a Comment