Saturday, January 12, 2013

Afanya Udaganyifu Mtihani Kwa Kutumia Saa ya iPod nano.

NewsImages/6758606.jpg
Picha ya Saa ya iPad nano iliyokamatwa
Sunday, January 13, 2013 12:27 AM
Mwanafunzi Mmoja nchini Misri amekatwa akiwa anafanya udanganyifu katika chumba cha mtihani kwa kutumia saa ndogo ya mkononi yenye uwezo wa kuhifani kumbukumbu inayotumia teknolojia ya iPod nano (smart wristwatch).
Katika hali isiyokuwa ya kawaida inayonesha matumizi mabaya ya teknolojia ya kisasa, Mwanafunzi aliyefahamika kwa jina la Petro Milad Hanna wa shule ya Sekondari ya Sita Oktoba iliyopo Mkoa wa Giza nchini Misri, amekamta baada ya kubuni mbinu mpya ya kufanya udanganyifu katika chumba cha mtihani kwa kutumia saa yake ya mkononi inayotumia teknolojia ya iPod nano.

Petro alibainika kutokana na kugeuka kwa mara kwa mara kumuangalia msimamizi aliyekuwa karibu yake, ndipo msimamizi huyo akagundua kuna jambo, alipopekuliwa alikutwa amevaa saa ndogo ya mkononi aina ya iPod nano, ikiwa imejaa majimu, Petro alitolewa darasani na kuwekwa kizuizini kwa muda na kisha kuruhusiwa kurudi nyumbani.

Kwa mujibu wa sheria za nchi hiyo mwanafunzi yoyote anayebainika anafanya udanganyifu katika mtihani anafutiwa mitihani yake yote na atasimamishwa masomo kwa kipindi kisichopungua mwaka mmoja.

Kufuatia kuibuka wimbi kubwa la wanafunzi wanaofanya udanganyifu katika mitihani kwa kutumia vifaa vya kisasa, wizara ya elimu ya nchini hiyo imeahidi kuweka kamera za ulinzi katika vyumba vya kufanyia mitihani ili kupambana na hali hiyo.

No comments:

Post a Comment