|
Friday, January 23, 2009 11:22 AM ZOEZI la udahili upya wanafunzi waliosimamishwa masomo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam limekamilika |
|
Zoezi hilo la udahili lilianza mapema mwa wiki hii la kusaili upya wanafunzi watakaoruhusiwa kurudi chuoni hapo. Wanafunzi wote walitakiwa kujaza fomu maalumu ambazo zitawaruhusu kurudi upya kuendeleza masomo yao pindi atakapojaza fomu hiyo maalumu vinginevyo hataruhusiwa kurudi chuoni hapo. Vilevile na kupatiwa vitambulisho vingine ili aweze kutambulika kama mwanafunzi wa chuoni hapo, na watatakiwa wavae vitambulisho hivyo ili aweze kuingia ndani ya chuo, japo utaratibu huo ulionekana kulalamikiwa kwa wanafunzi walio wengi na kuuita utaratibu wa kuvaa viambulisho ndipo uingie kwenye lango la chuo ni sawa na utaratibu wa “kipande system”. Pia ikiwemo na kukamilisha vipengele vyote vilivyowekwa kwenye fomu hizo. Katika udahili huo wakati unaendelea wanafunzi wapatao 2000 walifutiwa udahili ikiwemo na kukamatwa wanafunzi wanne kupinga kufutiwa kwa udahili wenzao. Kesho wanafunzi wa Vyuo Vikuu vya Umaa vya Elimu ya juu nchini wanatarajiwa kufanya maandamano ya kupinga kufutiwa kwa udahili kwa wanafunzi wenzao 2000 na vilevile kupinga sera ya uchangiaji. |
Saturday, January 12, 2013
Usaili Chuo Kikuu Wamalizika, Maandamano Makubwa Kesho
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment