
Wanafunzi
wa Chuop Cha Uongozi wa Fedha cha jijini Dar es Salaam (IFM) wakiwa
mbele ya geti la Wizara ya Mambo ya ndani walipovamia leo majira ya saa
nne nanusu asubuhi wakiwa na madai ya kutopewa ulinzi na jeshi la polisi
kwenye makazi yao ya Hosteli za Kigamboni kutokana na kuvamiwa na
majambazi mara kwa mara. Wanafunzi hao walidai siku ya Ijumaa walifanya
kikao na jeshi hilo ili wawape ulinzi lakini suala la ajabu siku
waliyofanya kikao na Jeshi hilo ndio siku waliovamiwa wenzao wawili
wakiume na kubakwa hali iliyosababishwa wanafunzi hao kubakwa.
Majambazi hao wamekua wakidai kupewa Laptop simu na fedha kama
mwanafunzi akikataa humfanyia vitendo vya kulawiti.

Kamanda
wa Polisi wa Kanda maalum ya Kipolisi ya jiji la Dar es Salaam Suleiman
Kova akimsikiliza Rais wa Serikali ya wanafunzi ya Chuo cha IFM mara
baada ya kuwasili eneo la ofisi za Wizara ya Mambo ya ndani ambapo
aliwaamuru wanafunzi hao wafuatane waende hadi Kigamboni kwenye Kituo
walichoripoti taarifa zao pamoja na kwenda kwenye Hosteli zao. Kova
aliahidi kushughulikia jambo hilo kwa haraka bila kusita.

Wakianza maandamano kuelekea Feli kwaajili ya kuvuka kwenda Kigamboni.

Kova akishangiliwa wakati wa safari kuelekea Feri

Kwenye kona ya feri kuwania geti ili waingie bure

Wakajazana kupita kiasi, Kova akazui kivuko kuondok hadi wapungue

Waligoma kupungua na kusababisha kivuko kutofanya kazi kwa zaidi ya saa 1.

Pamoja
na kutakiwa kupungua hapa wengine walizidi kuendelea kuingia na
kukijaza kivuko hicho. hii ni sehemu ya kwanza tutawaletea sehemu ya
pili ya tukio hili ambalo hadi hivi sasa filamu inaendelea hapa feli na
ikielekea Kigamboni.
Ila walifanikiwa na kuvushwa kuelekea upande wa kivukoni. Tutawajuza nini kiliendelea huko.
No comments:
Post a Comment