Tuesday, March 12, 2013

Afrika Kusini: Mtoto wa miaka 9 amuoa bibi wa miaka 61


Huyu mtoto anasema wazee wa zamani ndio walimuamrisha aoe lakini pamoja na hilo, hawajasaini cheti cha ndoa na wala hawaishi pamoja ambapo wazazi wa huyu bwana harusi walichangia harusi kwa kutoa euro 1500 ambazo walisisitiza ni kama matambiko na sio kisheria.
Mtoto huyu aitwae Sanele amekaririwa akisema “nilimwambia mama yangu, nahitaji kweli kuoa na nimefurahi nimemuoa Helen lakini nikikua nitaoa mwanamke wa umri wangu”
Mama mzazi wa Sanale anasema “babu yake ndio alimchangulia Sanale amuoe Helen kwa sababu yeye(Babu) anampenda, na wamefanya hivyo ili kutimiza maagizo ya wazee wa koo ambao wameshafariki, yani ni kama matambiko”. Maelezo na millardayo.com



No comments:

Post a Comment